Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wametakiwa kujiepusha na tabia na mienendo isiyofaa ambayo itawapelekea kwenye maambukizi ya virusi vya ukimwi na ugonjwa wa ukimwi.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Sipora Liana leo tarehe 12 Februari, 2020 wakati akifungua mafunzo ya VVU/UKIMWI pahala pa kazi kwa watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam yaliyofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mafunzo hayo yaliyokuwa katika mtindo wa majadiliano kati ya washiriki na wawezeshaji pamoja na utoaji wa mifano hai, yaliwavutia na kuwajengea uwezo watumishi hao wa umma kiasi cha wengi wao kuuliza maswali na kupatiwa ufafanuzi kutoka kwa wawezeshaji.
Wataalamu hao wa afya walitoa msisitizo kwa kila mtumishi wa umma kujijengea utaratibu wa kupima afya mara kwa mara, kubadili mitindo hatarishi ya maisha na kufanya mazoezi ya mwili ili kuepuka kuambukizwa au kuambukiza virusi vya UKIMWI pamoja na magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza yakiwemo Kisukari na Shinikizo la juu la damu.
Mafunzo hayo yameratibiwa Kitengo cha Maendeleo ya Jamii na Idara ya Afya ikiwa ni utekelezaji wa moja ya malengo ya Mpango Mkakati wa kutokuwa na maambukizi ya VVU ambayo Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imejiwekea.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.