Katika kuhakikisha inaongeza ari ya kujituma na kuwajibika kwa ipasavyo, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Ofisi ya Mganga Mkuu, imewapongeza baadhi ya watumishi wa kada ya afya waliofanya vizuri zaidi katika kutimiza majukumu Yao Kwa kuwapa zawadi mbalimbali.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wauguzi hao iliyofanyika kwenye Hospitali ya Mnazi Mmoja, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Dkt. Elizabeth Nyema amesema kuwa licha ya kuwepo Kwa watumishi wengi wanaofanya kazi vizuri lakini ofisi yake imeona ni vyema iwatambue wachache waliofanya vizuri zaidi.
"Tunatoa Motisha hii kama sehemu ya kutambua kazi kubwa inayofanywa na wauguzi wote na hii ikawe sababu ya kuendelea kutujengea umoja na mshikamano baina yetu. Tuna kila sababu ya kujipenda wenyewe na ndio maana leo tupo hapa kuwapongeza wale mliowajibika zaidi, haimaanishi kwamba wengine hawafanyi vizuri bali kwenye mafanikio ya wengi yupo Mmoja aliyefanya vyema zaidi". Amesema Dkt Elizabeth.
Naye mmoja kati ya Wauguzi waliopokea Pongezi hizo kutokana na kuonesha ufanisi mzuri kutoka katika Kitengo Cha Gari la Wagonjwa (Ambulance) nesi Beatrice Zacharia, ameshukuru Ofisi ya Mganga Mkuu kwa kutambua kazi yake na kwamba zawadi aliyopokea imempa moyo wa kuendelea kujituma zaidi.
"Kwakweli sikutegemea kama siku moja nitakuja kutambulika. Hii zawadi imenitia moyo sana hata kwa wenzangu pia kuona kumbe kazi yetu inatambulika". ameema nesi Beatrice.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.