Wazazi na Walezi wametakiwa kuzingatia lishe ya watoto ili kupata mlo kamili ambao unasaidia katika kujenga, kulinda na kuimarisha afya zao na kuepuka kushambuliwa na maradhi.
Wito huo umetolewa na Diwani wa Kata ya Jangwani Mhe. Zakaria Digossi alipohudhuria siku ya lishe kwa Kata ya Jangwani iliyofanyika kwenye Shule ya Msingi Mnazi Mmoja ikiwa ni sehemu ya kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alilolitoa tarehe 30 Septemba, 2022 wakati akihutubia Mkutano wa Mwaka wa Tathmini ya Sita ya Mkataba wa Lishe uliofanyika Jijini Dodoma kuwataka Wakuu wa Mikoa kuongeza jitihada za utekelezaji wa shughuli za lishe bora na kuzipa kipaumbele. " Kwa haya mafunzo mliyopata leo muende majumbani mkawaambie wazazi na walezi wenu kuwa tunatakiwa kupata mlo kamili kila siku. Lakini pia Niwapongeze Maafisa Lishe kwa kujituma kwao na kuhakikisha wanapita Kata kwa Kata kutoa elimu ya lishe." Amesema Mhe. Digossi
Naye, Afisa Lishe Bi. Neema Mwakasege amesema huu ni muendelezo wa kutekeleza mpango wa kutoa Elimu ya lishe bora, masuala ya uzazi pamoja na ukatili wa kijinsia kwa Wazazi, Walezi na Watoto katika Kata 36 na Mitaa 159 ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.