Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Mizengo Kayanza Pinda leo tarehe 4 Agosti, 2022 amelitembelea banda la maonesho ya nane nane la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na kujionea teknolojia mbalimbali zinazohusiana na Sekta za Kilimo, mifugo na uvuvi.
Akiwa ndiyeMgeni Rasmi wa Ufungizi wa maonesho ya nane nane kanda ya Mashauri yenye kauli mbiu : Ajenda 10/30, Kilimo ni biashara, shiriki kuhesabiwa, kwa mipango bora ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ” yanayohusisha mikoa minne ambayo ni Dar es Salaam, Morogoro, Pwani na Tanga, Waziri Mkuu Mstaafu Pinda ameridhishwa na teknolojia mbalimbali alizoziona katika banda la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Teknolojia ya upimaji wa udongo ili kuweza kujua afya ya udongo ni moja wapo ya teknolojia aliyojionea ambayo Halmashauri ya Jiji ina kituo cha Maabara katika kituo cha mafunzo cha Pugu Pugu Kinyamwezi.
Aidha Waziri Mkuu Mstaafu ameweza kujione teknolojia ya uzalishaji, usindikaji na ukaushaji wa Matunza ambayo ipo pia katika kituo cha Shamba darasa Pugu Kinyamwezi cha Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inayotumiwa na kikundi cha Upendo kwa wote ambacho kimewezeshwa na Halmashauri.
Vile vile ameridhishwa na namna Halmashauri inavyotenga 10% ya mapato yake ya ndani kuwawezesha wadau wa Kilimo, mifugo na Uvuvi ambapo amejione bidhaa mbalimbali za wajasiriamali zinazotokana na mazao yatokanayo na sekta husika.
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika mwaka wa fedha wa 2021/22 iliweza kutoa 5.6 Bilioni na katika mwaka wa fedha wa 2022/23 ina mpango wa kutoa 6.4 Bilioni ili kuendelea kuongeza mnyororo wa thamani na kukuza Uchumi wa vikundi vyao.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.