Na: Shalua Mpanda
Wataalamu kutoka zaidi ya nchi saba za Afrika wamekutana mjini Zanzibar kujadili taarifa za fedha za miaka mitano kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Katika Mkutano huo uliohusisha wataalam mbalimbali wakiwemo wachumi, Ofisi ya Rais -TAMISEMI, Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mkoa wa Dar es Salaam na Taasisi nyingine za Serikali, una lengo la kuzitumia taarifa hizo katika kuboresha huduma mbalimbali za Jamii Jijini humo na katika maeneo mengine.
Akizungumza katika Mkutano huo ndugu Gaston Makwembe aliyemwakilisha mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Mhe. Omary Kumbilamoto, amesema kutokana na changamoto iliyoikumba Dunia kutokana na ugonjwa wa UVIKO-19, nchi nyingi ikiwemo Tanzania uchumi wake uliathirika.
Amesema kutokana na changamoto hiyo ndipo Taasisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Uchumi wa Afrika (UNECA) ikaamua kuliteua Jiji la Dar es salaam kupitia taarifa zake za fedha kwa kipindi cha mwaka 2018/19 hadi 2021/2023 ili kuweza kutoka na suluhisho litakalowezesha Jiji hilo na mengine barani Afrika kuweza kuwa imara kiuchumi hata mara baada ya majanga kutokea kama ilivyokuwa kipindi cha UVIKO-19.
"Halmashauri yetu ya Jiji ni moja kati ya Halmashauri zilzokumbwa na changamoto ya kushuka kwa mapato katika kipindi cha UVIKO-19 kutokana na shughuli nyingi kusimama ikiwemo sekta ya utalii ambayo inatuingizia fedha nyingi kupitia Hotel Levy(ushuru wa biashara ya hoteli)". Alisema Bw. Makwembe
Kikao hicho kimehudhuriwa na wataalamu kutoka miji ya Younde Cameroon, Adis Ababa Ethiopia, Kigali Rwanda, Nairobi Kenya,Lusaka Zambia na wenyeji Tanzania huku waheshimiwa Mameya wa majiji ya Dar, Nairobi na Zanzibar wakihudhuria pia Mkutano huo.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.