Na: Shalua Mpanda
Kukamilika kwa Mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya Shilingi bilioni 36.8 unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) kutawezesha wakazi zaidi ya laki nne na elfu hamsini wa majimbo ya Ukonga na Segerea kuondokana na kero ya upatikanaji wa huduma ya maji katika maeneo hayo.
Hayo yameelezwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA,Mhandisi Mkama Bwire wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa(CCM) ya wilaya ya Ilala iliyofanyika leo Februari 19,2025.
Mhandisi Bwire amesema mradi huo umefikia asilimia 99 na kinachosubiriwa kwa sasa ni kuyaruhusu maji hayo kwenda kwa Wananchi zoezi ambalo litakamilika hivi karibuni.
"Mradi huu umefikia asilimia 99,ninawahakikishia wananchi kuwa katika muda wa siku tatu watapata huduma ya maji". Alisema Mhandisi huyo.
Aidha, ameongeza kuwa mradi huo wa maji una uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 9 ambazo zitaweza kumudu mahitaji ya wakazi wa kata zaidi ya kumi wa majimbo hayo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ilala Alhaj Said Sidde amempongeza Mtendaji huyo wa DAWASA kwa kuweza kusimamia vizuri fedha za mradi huo ambao utaenda kumaliza kabisa changamoto ya maji.
Ziara hiyo ambayo pia Mkuu wa Wilaya Ilala Mhe. Edward Mpogolo alihudhuria,ilikuwa na lengo la kukagua miradi ya maendeleo na kuangalia utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.