Viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika picha ya pamoja na wenyeviti wa kamati za kudumu za Manispaa ya Strängnäs baada ya mkutano wao uliofanyika Aprili 3, 2017 katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Strängnäs. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Watoto na Elimu, Maria Ehrnfeldt, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Ingrid Fäldt, Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii, Monica Lindell Rylen, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sipora Liana, Mwenyekiti wa Manispaa ya Strängnäs, Jacob Hogfeldt, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni, Maabad Hoja, Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi na Miundombinu, Sixten Skullman na mratibu wa mradi wa mawasiliano wa “Youth Democracy”, Helena Edvisson.
Manispaa ya Strängnäs (Strängnäs kommun) nchini Sweden katika Jimbo la Södermanland, kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA), ilitoa mwaliko kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kushiriki katika mafunzo nchini Sweden yaliyohusu “Exchange Program: Municipal Partnership” kwa lengo la kujifunza mafanikio ya mji wa Strängnäs katika mfumo wake wa elimu unaowashirikisha wanafunzi na vijana ambao wapo katika shule za awali, shule za msingi na sekondari katika kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo ya mji wa Strängnäs kupitia mabaraza ya wanafunzi/vijana ikiwa ni pamoja na kuwaandaa kuwa viongozi wa nafasi mbalimbali chini ya mradi wa “Youth Democracy”.
Manispaa ya Strängnäs yenye wakazi 34,000 imeonesha nia ya kushirikiana na Jiji la Dar es Salaam kujengea uwezo vijana na kuendeleza vipaji vyao katika shule za awali, msingi na sekondari kwa kuanzisha mabaraza ya wanafunzi/vijana(Pupils/Youth Councils) chini ya mradi wa “Youth Democracy” kwa ufadhili wa SIDA. Mafunzo hayo ni hatua ya mwanzo “inception phase” yaliyokuwa na lengo la kuiwezesha Dar es Salaam kupata uelewa wa dhana ya “Youth Democracy” na kufanya maandalizi ya utekelezaji wake.
Menejimenti ya Manispaa ya Strängnäs ikijadiliana na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Bi. Sipora Liana, katika mkutano uliofanyika Aprili 1, 2017 katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Strängnäs kuhusu utekelezaji wa mradi wa “Youth Democracy” katika Jiji la Dar es Salaam
Ujumbe wa Dar es Salaam ukipokea maelezo kutoka kwa mmoja wa walimu wa sanaa na utamaduni wa chuo cha utamaduni cha Manispaa ya Strängnäs nchini Sweden wakati wa ziara yao ya mafunzo
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.