• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

ZIARA YA MKUU WA WILAYA YA ILALA KATIKA KATA YA PUGU-GONGO LA MBOTO YATOA NJIA UTATUZI WA CHANGAMOTO YA MAJI.

Tarehe iliyowekwa: May 26th, 2021

ZIARA YA MKUU WA WILAYA YA ILALA KATIKA KATA YA PUGU - GONGO LA MBOTO YATOA NJIA UTATUZI WA CHANGAMOTO YA MAJI.

Na Amanzi Kimonjo.

Mkuu wa wilaya ya Ilala Mhe.Ngw’ilabuzu Ndatwa Ludigija tarehe 26 mei 2021 ametembelea mradi wa ujenzi wa tanki na mfumo wa usambazaji wa maji uliopo Pugu-Gongolamboto Jijini Dar Es Salaam tenki ambalo linachukua ujazo wa lita milioni mbili ambalo limeshakamilika kwa asilimia mia moja na zoezi la usambazaji wa maji umeanza kwa kata ya Pugu maeneo ya Buyuni, Majoe, Gongo la mboto, Pugu Stesheni,na sehemu ndogo ya Chanika huku wananchi  wakifurahia huduma ya maji na baadhi yao wako katika utaratibu wa kusambaziwa maji.

Hata hivyo, Mradi huu unaotoa bomba kuu la kusambaza maji lenye urefu wa kilomita 13.5 kutoka Kisarawe mpaka Ukonga Air wing pamoja na tenki lenye ujazo wa lita milioni mbili likiambatanishwa na mabomba madogo yenye upana wa  ‘inch’ tatu hadi nane ya kusambaza maji  katika Kata hizo yakiwa yamekamilika kwa asilimia mia moja.

Aidha, Mkuu wa wilaya Mhe. Ludigija amesema “Natoa pongezi kwa  Mamlaka ya Maji Safi na Salama Dar es Salaam (DAWASA) kwa kuwezesha usimamizi na taratibu za usambazaji wa maji, kubwa zaidi kwa Wilaya ya Ilala ninatamani mradi huu uwe sehemu ya wananchi kupata maji na kuondokana na adha ya maji”. Hivyo tatizo la muda mrefu la ukosefu wa maji kwa kata ya Pugu-Gongolamboto litakua historia baada ya mda mchache.

Vile vile, Msimamizi wa mradi huu Mhandisi Ishumaili Kakwezi amesema “usambazaji wa maji unaendelea kwa mahitaji ya wateja na mpaka sasa tumewafikia wateja 2000 na wengine tunawaungia mabomba lengo huduma hii ya maji iwafikie kwa uharaka”.

Kwa upande mwingine Mkuu wa Wilaya Mhe.Ludigija alitembelea  mradi wa ujenzi wa daraja  la Ulongoni A na Ulongoni B iliyoko chini ya mradi mkubwa wa DMDP ambapo ujenzi wa daraja la Ulongoni A uliogharimu shilingi billion 4.5 umefikia  asilimia 79 na inategemewa kufikia mwezi wa sita wananchi wataanza kutumia daraja hilo,  huku daraja la Ulongoni B lililo gharimu takribani shilingi billion 2.5  ujenzi bado unaendelea.

“Ninamshukuru Mkurugenzi wa  Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam,  wataalamu wetu wakiongozwa na Mhandisi Magori, Mkandarasi na wengine walioshiriki katika kufanikisha ujenzi huu kwa hatua ulipofikia maana naona matumaini kua ifikapo tarehe 10 mwezi wa sita wananchi wataanza kutumia daraja hili  na inafahamika mradi huu utamalizika tarehe 30 mwezi wa sita na nitoe wito kwa wataalamu wa Jjiji,mkurugenzi,mkandarasi,Tarura, waongeze kasi ya ujenzi huu nafarijika kuona jinsi kazi inavyoendelea  na tutafuatilia mpaka hapo mradi huu utakapo malizika”.

Akitoa shukrani zake kwa viongozi Mhandisi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mhandisi .Magori amesema “Mradi huu wa ujenzi wa Daraja la ulongoni unaendelea na kwa niaba ya Halmashauri tunamshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa pesa kuendeleza mradi huu pamoja na  viongozi wetu Wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na Katibu tawala wa Wilaya ya Ilala kwa kuonyesha ushirikiano wao wa kutembelea  na kuifatilia miradi hii toka imeanza mpaka hapa ilipofikia”.

Ziara hii  ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala iliweza kumalizika kwa kutembelea ujenzi wa stendi ya Kinyerezi  unaombatana na ujenzi wa barabara kutoka ulongoni B hadi kufika katika stendi  hiyo ya Kinyerezi  ambapo barabara hiyo yenye kilometa 9.5 ikiwa inaendelea kujengwa kwa kiwango cha lami.

Ukamilifu wa  Stendi hii ya Kinyerezi ambayo ni kitovu  cha biashara na shughuli nyingine za kiuchumi  inategemewa na wananchi wa Kinyerezi pamoja na wananchi wa maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar es salaam kwani ipo karibu na stendi kuu ya mabasi ya  kwenda mkoani (Stendi ya Magufuli )hivyo basi itarahisisha wananchi wote wa Ilala kuweza kufika na kupata huduma.

Akihitimisha ziara yake  Mkuu wa Wilaya  ya Ilala Mhe. Ludigija amesema “Mkandasi pamoja na wasaidizi wake wasibweteke kwa sifa hizi tunazowapatia bali wafanye kazi na waongeze kasi wasiseme Mkuu wa Wilaya amepita na kazi isimame nataka hadi kufikia tarehe 30, Juni 2021 kazi hii iwe imekamilika kama ilivyokusudiwa.”

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.