Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam ndugu Elihuruma Mabelya amewataka Watumishi walioteuliwa kusimamia zoezi la uandikishaji katika Daftari la Wapiga Kura la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa litakaloanza Oktoba 11,2024 kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wafuate sheria na taratibu zilizopo.
Ameyasema hayo leo Oktoba 7, 2024 wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa waandikishaji wapiga kura yaliyofanyika katika ukumbi wa Anatouglo jijini humu.
Mkurugenzi Mabelya amesema anaamini kuwa Wasimamizi hao wana uwezo mkubwa wa kufanya zoezi hilo liwe na mafanikio makubwa pia amewataka kujiamini na kutanguliza maslahi ya Taifa mbele.
"Hakikisheni mnasimamia matakwa ya kisheria yanayosimamia Uchaguzi na epukeni yale yote yanayoweza kukwamisha zoezi hili". Alisema.
Aidha, Mkurugenzi huyo amewataka Wasimamizi wa zoezi hilo kushirikiana na Vyama vya Siasa kwenye mambo yanayopaswa kushirikishwa ili kuweka uwazi katika zoezi hilo.
Awali kabla ya ufunguzi wa Mafunzo hayo,Wasimamizi hao walikula kiapo cha utii katika kuelekea zoezi hilo linalotarajiwa kuanza Oktoba 11 mwaka huu.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.