Benki ya Biashara ya Dar es Salaam ilianzishwa mwaka 2002 kufuatia wito wa Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Benjamin William Mkapa. Malengo ya uanzishwaji wake yakiwa ni kuwapatia mitaji wananchi wenye kipato cha chini na cha kati ambayo itasaidia kuanzisha na kuendeleza biashara zao.
Hadi sasa Benki ya Biashara ya Dar es Salaam imefanikiwa kuanzisha jumla ya matawi nane, saba yakiwa jijini Dar es Salaam na moja likiwa jijini Dodoma.
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na Manispaa za Ilala, Kinondoni na Temeke ni wanahisa waanzilishi wa Benki ya Biashara ya Dar es Salaam, huku Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ikiwa inamiliki hisa 6,832,094 zenye thamani ya shilingi 2,732,837,600.00 kwa bei ya shilingi 500 kwa bei ya soko la hisa tarehe 30/06/2016.
Kitega Uchumi hiki kina tija kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kuwa kinaongeza mapato kwa kutoa gawio.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 2128800
Namba ya Mkononi:
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.