Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imefanikiwa kuimarisha utalii jijini kwa kununua "Luxurious Bajaj" na Basi la Utalii. Magari haya yanafanya biashara ya kuendeleza utalii jijini Dar es Salaam kwa kukodiwa na watalii.
Pia Halmashauri imefungua ofisi ya Utalii eneo la “Nyerere International Airport Terminal II na Terminal III".
Ofisi hizi zinatumika kutoa taarifa mbalimbalil za vivutio vya utalii kwa wageni mbalimbali wanaoingia jijini.
Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ilitenga kiasi cha jumla ya shilingi 300,000,000 kwa ajili ya kununua basi lingine la utalii aina ya ‘Double-deck’ kwa ajili ya kutembeza watalii katika vivutio mbalimbali vya utalii Jijini ‘Dar City Tour”. Hatua ya manunuzi ya basi hili zinaendelea ambapo ‘specifications’ za basi hilo zimetumwa kwa wazabuni ‘suppliers’.
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam tayari imepata mpangaji kwa ajili ya kuendesha Mgahawa husika pamoja na eneo la bustani pembeni ya jengo la Old Boma. Mgahawa umeanza kazi rasmi tarehe 05 Julai, 2019.
Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ilikabidhiwa eneo la fukwe la Barabara ya Barack Obama na Mhe. Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan siku ya mazingira Duniani tarehe 05 Juni, 2018 ili kuliendeleza, kuliboresha na kulifanya kivutio cha utalii.
Katika kutekeleza agizo hilo Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ilitenga kiasi cha shilingi 200,000,000.00 kwa ajili ya kutengeneza eneo la maegesho ya magari (Parking), kuweka vioski vya kuuzia chakula (Mobile containers), kutengeneza bustani na kuendelea kutunza miundombinu iliyopo maeneo hayo ikiwemo ukuta (Sea wall), choo cha umma na fukwe. Maandalizi ya awali ya utengenezaji wa “Pavement blocks” kwa ajili ya eneo la maegesho na vioski vya kuuzia chakula yameanza.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.