Friday 22nd, November 2024
@Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Kila tarehe 5 Juni, kila mwaka Watanzania tunaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani. Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliamuliwa na Baraza la Umoja wa Mataifa la mwaka 1972, wakati wa mkutano wa kwanza wa Umoja wa Mataifa uliohusu Mazingira huko Stockholm, nchini Sweden.
Aidha, Azimio la kuunda Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia Mazingira Duniani, yaani United Nations Environment Programme (UNEP) lilipitishwa pia siku hiyo. Tangu wakati huo, nchi mbalimbali duniani zimekuwa zikiadhimisha Siku ya Mazingira Duniani kila mwaka tarehe 5 Juni, kwa ujumbe maalumu unaotolewa na Umoja wa Mataifa.
Madhumuni ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ni kuhamasisha jamii duniani kote kuelewa masuala yahusuyo Mazingira na pia kuhamasisha watu wa jamii mbalimbali duniani kuwa mstari wa mbele katika kuchukua hatua za kuhifadhi na kulinda mazingira. Aidha, tunatumia siku hii kutoa fursa kwa jamii kufahamu kwamba wao wana wajibu wa kuzuia madhara na mabadiliko hasi katika Mazingira na kuhamasisha jamii kufanya mazingira yao kuwa salama na masafi katika maisha yetu na vizazi vyetu.
Kimataifa maadhimisho haya yanafanyika nchini India katika mji wa New Delhi. Kaulimbiu inayoongoza maadhimisho haya ni “Beat Plastic Pollution”. Kaulimbiu hii inahimiza jamii kuepuka uchafuzi wa mazingira utokanao na plastiki. Maamuzi ya kupeleka maadhimisho haya nchini India ni kutokana na nchi ya India kuweka juhudi katika kupunguza uchafuzi wa mazingira utokanao na plastiki kwa kutumia mbadala wa plastiki na kurejeleza taka za plastiki. Aidha, India ni moja ya nchi zilizo mstari wa mbele katika kurejeleza taka za plastiki. UNEP imeamua India iwe mwenyeji wa maadhimisho haya kimataifa ili kutoa fursa kwa nchi nyingine kwenda India kujifunza kupunguza uchafunzi utokanao na plastiki na kurejeleza taka za plastiki.
Pamoja na kauli mbiu ya kimataifa, kauli mbiu yetu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira mwaka huu kitaifa ni "Mkaa Gharama; Tumia Nishati Mbadala”.
Maadhimisho haya Kitaifa yatafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.