• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani

Friday 16th, May 2025
@Viwanja vya Mnazi Mmoja

Kila tarehe 5 Juni, kila mwaka Watanzania tunaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani. Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliamuliwa na Baraza la Umoja wa Mataifa la mwaka 1972, wakati wa mkutano wa kwanza wa Umoja wa Mataifa uliohusu Mazingira huko Stockholm, nchini Sweden.

Aidha, Azimio la kuunda Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia Mazingira Duniani, yaani United Nations Environment Programme (UNEP) lilipitishwa pia siku hiyo. Tangu wakati huo, nchi mbalimbali duniani zimekuwa zikiadhimisha Siku ya Mazingira Duniani kila mwaka tarehe 5 Juni, kwa ujumbe maalumu unaotolewa na Umoja wa Mataifa.

Madhumuni ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ni kuhamasisha jamii duniani kote kuelewa masuala yahusuyo Mazingira na pia kuhamasisha watu wa jamii mbalimbali duniani kuwa mstari wa mbele katika kuchukua hatua za kuhifadhi na kulinda mazingira. Aidha, tunatumia siku hii kutoa fursa kwa jamii kufahamu kwamba wao wana wajibu wa kuzuia madhara na mabadiliko hasi katika Mazingira na kuhamasisha jamii kufanya mazingira yao kuwa salama na masafi katika maisha yetu na vizazi vyetu.

Kimataifa maadhimisho haya yanafanyika katika mji wa Hangzhou nchini China na kaulimbiu ya Kimataifa inayoongoza maadhimisho haya ni “Uchafuzi wa Hewa” (Air Pollution). Kaulimbiu hii inahimiza jamii kuepuka shughuli zinazo sababisha uchafuzi wa hewa. Maamuzi ya kupeleka maadhimisho haya China ni kutokana na nchi ya China kuwa na viwanda vingi ambavyo uzalishaji wake unasabisha uchafuzi wa Hewa. Hivyo, maadhimisho haya yanatoa fursa kwa nchi ya China na nchi nyingine duniani kuhamasika kuepuka shughuli zinazosababisha uchafuzi wa mazingira na kuwaepusha watu wake na maradhi yatokanayo na uchafuzi wa hewa.

Mwaka huu hapa nchini hatutakuwa na maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira Duniani  na badala yake kila Mkoa utafanya shughuli za maadhimisho katika maeneo yake kwa kuzingatia kaulimbiu ya maadhimisho haya isemayo: “Tumia mifuko mbadala wa Plastiki; kwa ustawi wa Afya, Mazingira na Maendeleo ya Uchumi”. Kaulimbiu hii ni mwitikio wa Taifa wa Tamko la Serikali la kukataza uzalishaji, uingizaji ndani ya nchi usambazaji na matumizi ya mifuko ya plastiki na kuhimiza wananchi kutumia mifuko mbadala. Tamko hili limetokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaotokana na utupaji ovyo wa mifuko ya plastiki ambayo imeleta madhara makubwa ya kimazingira, afya za viumbe hai, ikiwemo binadamu wanyama, pamoja na kuathiri uchumi  wa nchi kwa ujumla. Aidha, mifuko ya plastiki imekuwa sehemu muhimu ya jamii yetu, lakini changamoto ya usimamizi na athari za taka za plastiki nchini na duniani inahatarisha mustakabali wa ustawi wa jamii, uchumi na mazingira kwa kuwa mifuko hii huchukua muda wa takriban miaka 500 kuoza.

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.