Na: Doina Mwambagi
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo tarehe 27 februari, 2025 limefanya mkutano wa robo ya pili ya katika ukumbi wa Arnatoglou na kupitisha taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi hicho.
Katika kikao hicho, Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Halmashauri waliwasilisha taarifa za kamati zao, ambapo wajumbe wa Baraza la Madiwani walizipokea na kuzipitisha ili zibaki kuwa kumbukumbu sahihi kwa Halmashauri.
Sambamba na hilo, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam iliwasilisha taarifa ya miradi inayotekelezwa na TARURA, ikiwa ni pamoja na mfuko wa barabara, tozo ya mafuta, mfuko wa jimbo, mapato ya ndani na miradi ya DMDP II katika Wilaya ya Ilala.
Akiwasilisha taarifa ya miradi hiyo, Mhandisi Magori amesema kuwa miradi yote inayotekelezwa kwa mapato ya ndani inaendelea kwa kasi, huku akiahidi kuwa itakamilika kwa wakati.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Ndugu Elihuruma Mabelya, amewashukuru watumishi wote wa Halmashauri pamoja na viongozi kwa kusimamia majukumu yao kwa kuakisi maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Pia amemshukuru Mstahiki Meya na Baraza la Madiwani kwa mchango wao katika maendeleo ya Jiji.
"Nathamini mchango na maoni ya Baraza hili, na naahidi kuyafanyia kazi maelekezo yenu kwa ustawi wa Jiji letu," alisema Mkurugenzi Mabelya.
Akihitimisha kikao hicho, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto, aliwashukuru Waheshimiwa Madiwani na Watendaji wa Halmashauri kwa kushiriki kikamilifu katika ziara za kamati mbalimbali za robo ya pili ya mwaka wa fedha.
Aidha Baraza limelidhia na kupitisha taarifa hizo.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.