KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM wa Taifa, CPA Amos Makalla, amewataka wakandarasi kukamilisha miradi kwa wakati huku akiwahimiza watendaji kuhakikisha wanasimamia kwa kasi utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili ikamilike kwa wakati.
CPA Makalla ametoa maagizo hayo leo Julai 09, 2024 Jijini Dar es Salaam akihitimisha ziara yake ya siku tatu katika Jimbo la Ilala ambapo alitembelea mradi wa ujenzi wa madarasa 20 ya ghorofa Shule ya Sekondari Mnazi Mmoja wenye thamani ya shilingi bilioni 1.8 pamoja na Mradi wa barabara zaidi ya 20 zinazotekelezwa katika Mitaa mbalimbali za Kata ya Ilala ikiwemo Mtaa wa Mwanza na Kigoma zitakazogharimu takribani shilingi bilioni 30 ikiwa ni fedha kutoka Serikali Kuu na fedha kutoka mradi wa DMDP.
Akiongea wakati wa ziara hiyo CPA Makalla ameeleza kuwa “Dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassani ni kuhakikisha anaboresha miundombinu yote kuanzia afya, elimu hadi barabara hivyo niwatake watendaji msimamie miradi hii kwa ukaribu ili ikamilike kwa wakati kwani fedha zipo. Pia niwatake wakandarasi kuhakikisha mnakamilisha ujenzi haraka kwani kupitia miundombinu hii tutakua tumetimiza dhamira ya Mhe. Rais ya kuboresha sekta ya elimu na miundombinu ya barabara”.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha katika Wilaya ya Ilala za utekelezaji wa miradi ya maendeleo huku akiwahakikishia wananchi wa Wilaya ya Ilala kuboreshewewa mazingira ya biashara kwani Jiji la Dar es Salaam limetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa masoko makubwa ya kisasa yatakayoenda kumaliza changamoto zote wanazozikabili.
Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Ndg. Jomaary Satura ameahidi kusimamia kwa ukaribu miradi hiyo ikamilike kwani fedha za kukamilisha miradi hizo zipo japo wakandarasi ndio wanachangamoto ila atahakikisha changamoto hizo anazitatua na miradi itakamilika kwa wakati.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.