Mkuu wa wilaya ya Ilala Mheshimiwa Edward Mpogolo leo Disemba 17, 2024 amekutana na kufanya kikao na wakandarasi pamoja na walimu wa Sekondari zinazotekeleza ujenzi wa miradi ya Sekondari.
Lengo la Kikao hicho ni kupanga mikakati ya kukamilisha Miradi hiyo ikiwa ni maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wanaoanza kidato cha kwanza mwaka 2025.
Katika kikao hicho Wakandarasi walipata nafasi ya kujadiliana changamoto mbalimbali na hatua za kuweza kuzitatua ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea.
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Elihuruma Mabelya pamoja na baadhi ya wakuu wa Divisheni na Vitengo kutoka Halmashauri ya Jiji hili walihudhuria pia kikao hicho.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.