Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mheshimiwa Edward Mpogolo, leo tarehe 8 Agosti 2025 ametembelea banda la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki yanayofanyika Mkoani Morogoro.
Akiwa kwenye ziara hiyo Mheshimiwa Mpogolo amesema Halmashauri ya hiyo inaendelea kushirikiana na wakulima na wafugaji na wavuvi ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo mbalimbali ili kuongeza tija, ubora wa mazao, na ustawi wa mifugo.
Mheshimiwa Mpogolo amewataka wananchi kuja kujifunza kilimo cha mjini huku akisisitiza kuwa kilimo cha mbogamboga kinaweza kufanyika kwenye maeneo madogo na kuchangia kipato cha familia.
Aidha, ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kuunga mkono kilimo cha mjini na kuchochea maendeleo ya kilimo na mifugo kwa wakazi wake.
“CHAGUA VIONGOZI BORA KWA MAENDELEO ENDELEVU YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI 2025”
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.