• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

DC Mpogolo awataka wafanyabiashara kuchangamkia fursa mkutano wa Wakuu wa Nchi Afrika

Posted on: January 19th, 2025

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amewataka wafanyabiashara Kariakoo kuchangamkia fursa katika Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaotarajiwa kufanyika Januari 27 na 28 mwaka huu.

Amesema Rais Dk. Samia, amekuwa kinara wa Dunia na Kinara wa Afrika katika matumizi ya nishati safi, hivyo kuanzia Januari 26  Tanzania itaanza kupokea wageni wakiwemo marais kutoka nchi za Afrika ambao watahudhuria mkutano huo.

Mhe. Mpogolo ameyasema hayo leo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, katika Bonza maalumu lililoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) likishirikisha wafanyabiashara wa Mkoa wa kikodi wa Kariakoo. 

“Ninawaomba wafanyabiashara  kujiandaa  kupokea wageni hawa.Mkutano huo utahudhuriwa na marais kutoka nchi nyingi za Afrika ambao watapenda kufika Kariakoo au kutuma wawakilishi wao hivyo ni vyema  wafanyabiashara wa Kariakoo kujiandaa kimataifa." ameeleza Mhe. Mpogolo.

Amesema ni wakati wa kuifanya Kariakoo  kuwa ya Kimataifa ambapo serikali itatoa mabango maalumu ya mkutano huo.

Aidha, Mhe. Mpogolo amebainisha Soko la Kariakoo ni tegemeo kubwa kwa Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam na taifa kwa ujumla katika ukusanyaji mapato  hivyo kuahidi ushirikiano mkubwa kwa wafanyabiashara na Mamlaka ya Mapato.

Aliishukuru TRA kwa ufanisi mkubwa ambapo ufanisi huo umeifanya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kukusanya sh. bilioni 101 katika mwaka wa fedha 2023/24 ambapo malengo ya awali yalikuwa ni kukusanya sh. bilioni 81 tu.

“Kwa kasi hii ya TRA katika ukusanyaji mapato Mwaka huu wa fedha  tutajiwekea malengo ya kukusanya hata sh. bilioni 120,” amesema Mhe. Mpogolo.

Ameeleza Serikali wilayani Ilala,  itaendelea kushirikiana na TRA na wafanyabiashara wote kwa sababu inatambua umuhimu wa kodi katika maendeleo ya miradi mbalimbali.

“Rais Dk. Samia, alitulietea zaidi ya sh. bilioni 350 za maendeleo Ilala. Tumefanikiwa kutekeleza miradi mingi, ikiwamo ya elimu, afya na barabara." Amebainisha.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo, Seveline Mushi, alisema wataendelea  kushirikiana na TRA na serikali kwa kulipa kodi kwa wakati.

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.