Na: Doina Mwambagi
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila amewataka wenyeviti wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es salaam kupunguza maneno katika uongozi badala yake wakawatumikie wananchi kwa kufanya kazi kwa bidii.
Ameyasema hayo leo tarehe 16 Desemba 2024, wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo elekezi kwa wenyeviti wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika katika ukumbi wa Golden Jubilee Jijini Dar es salaam.
Akiongea katika mafunzo hayo, Mhe. Chalamila amewataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kuwatumikia wananchi kwa kwa kuzingatia na kutekeleza falsafa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni Maridhiano, ustahimilivu, mageuzi na kujenga taifa upya (4Rs).
“Imani mliyopewa na wananchi ni kubwa sana hivyo mna deni la kuwatumikia kwa kufanya kazi kwa bidii pia kuwaongoza kwa haki ikiwa pamoja na kokomesha migogoro ya Ardhi katika mitaa yenu”. Ameeleza Mhe. Chalamila.
Aidha, Mhe. Chalamila ametoa maelekezo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha wanatoa mafunzo kwa wenyeviti wa Mitaa katika kila Halmashauri na kusisitiza mafunzo hayo yafanyike kwa muda uliopangwa.
Awali akifungua mafunzo Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Toba Nguvila amesema Serikali imeadhimia kutoa mafunzo kwa wenyeviti wa Serikali za Mitaa lengo ikiwa ni kuwapatia stadi za kazi ili waweze kuongoza vyema.
Mafunzo hayo yatafanyika kwa muda wa siku mbili kwanzia tarehe 17 hadie18 Decemba 2024, kwa Halmashauri zote za mkoa wa Dar es Salaam.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.