Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Elihuruma Mabelya amesema kuwa wanakwenda kufungua tenda ambayo itakwenda kufanya mabadiliko katika bonde la Mto Msimbazi kuhusu muonekano na mazingira yake kiujumla.
Ameyasema hayo Januari 15, 2025 wakati wa hafla ya ufunguzi wa zabuni ya ujenzi wa mradi wa mto Msimbazi, uliofanyika katika ukumbi wa TAMISEMI uliopo katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam.
Aidha, amesema kuwa tenda hiyo ilitangazwa kwa ajili ya kuwapata wazabuni kutoka kampuni mbalimbali watakaoweza kutekeleza mradi huo na kuwatakia kila la heri wale ambao watafanikiwa kuchaguliwa kwa ajili ya kutekeleza mradi huo.
Katika hatua nyingine Mabelya amewataka wazabuni watakao shinda tenda hiyo wafanye kazi kwa weledi kwa kuzingatia maslahi ya nchi na jiji la Dar es Salaam kwani mradi huo unamaslahi mapana ya kitaifa hivyo wataendelea kufuatilia kwa makini ili aweze kupatikana mwenye uwezo mkubwa wa kutekeleza mradi huo.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.