• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Hafla ya kutia saini Mkataba wa Ushirikiano wa majiji ya Hamburg na Dar es Salaam

Posted on: November 14th, 2017

DAR ES SALAAM na Hamburg zimefungua ukurasa mpya wa uhusiano wao wa Miji Dada kwa kusaini mkataba mpya wa uhusiano kati yao. Mkataba huo umesainiwa Novemba 14, mwaka huu katika Jiji la Hamburg na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita na Mstahiki Meya wa Jiji la Hamburg, Olaf Scholz, ukishuhudiwa na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sipora Liana, watendaji wakuu wa mamlaka ya Jiji la Hamburg na taasisi mbalimbali za Serikali katika Jiji hilo, wawakilishi wa asasi za kiraia na baadhi ya Watanzania wanaoishi Hamburg. 

Mkataba wa awali wa uhusiano huo ulitiwa saini mwaka 2010 na Adam Kimbisa na Ole Van Beust waliokuwa mameya wa majiji hayo katika kipindi hicho.

Mstahiki Meya na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam waliwasili katika Jiji la Hamburg kwa ziara ya kikazi na kusaini mkataba huo wakitokea katika mji wa Bonn ambako walishiriki katika mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi ulioandaliwa na taasisi ya Engagement Global ya Ujerumani kwa miji washirika wa Ujerumani. 

Viongozi hao wawili wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wakiwa mjini Bonn walishiriki pia katika mkutano wa mameya na magavana ambao ulikuwa sehemu ya mkutano ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa wa COP23 ambao umefanyika sambamba na mkutano ulioandaliwa na Engagement Global.

Kabla ya kusainiwa kwa mkataba huo, vikao vya wataalam mbalimbali wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Engagement Global, miji wa shirika na wataalam wa Wizara ya Maendeleo ya Miji na Makazi wa Jiji la Hamburg, vilifanyika mjini Bonn na Hamburg kwa usimamizi wa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam na Mtendaji Mkuu wa Jiji la Hamburg,Wolfgang Schmidtz, kubaini maeneo mengi zaidi ya ushirikiano kati ya miji hiyo, wahusika na miradi mipya inayoweza kutekelezwa kwa ufanisi na kwa manufaa ya wananchi kupitia uhusiano huo.

Pande hizo mbili, hasa kwa kuzingatia matakwa ya Dar es Salaam, zimekubaliana kushirikiana katika maeneo mabadiliko ya tabia nchi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa umma kuhusu namna ya kukabiliana na mabadiliko hayo, upangaji wa miji, uboreshaji wa huduma za usafiri wa umma na shughuli za kukuza utalii katika Jiji la Dar es Salaam.

Baada ya kusainiwa kwa mkataba huo, viongozi hao wa Jiji la Dar es Salaam walikutana na Bodi ya Ushauri ya Jiji la Hamburg na kisha kuwa na mkutano mwingine na wadau wa uhusiano huo wakiwemo Watanzania wanaoishi Hamburg ambao wajumbe wote kwa ujumla walisisitiza kila upande ufanye jitihada za dhati za kuimarisha ushirikiano huo kwa kuacha urasimu, kutojihusisha na vitendo vya rushwa, kuwa wawajibikaji zaidi na kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kuwa na Tanzania ya viwanda.

Hii ni safari ya kwanza ya kikazi nje ya nchi kwa Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita na Mkurugenzi wa Jiji hilo, Sipora Liana, kusafiri pamoja na kurejea nchini wakiwa wamefanikiwa katika kutimiza malengo ya safari yao mjini Bonn na Hamburg.

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.