• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam yajipanga kikamilifu kukabiliana na magonjwa ya mlipuko

Posted on: December 21st, 2022

Magonjwa ya mlipuko ni magonjwa ambayo hutokea kutokana na maambukizi ya ugonjwa fulani na kwa kawaida huenea haraka na kuathiri watu wengi kwa kipindi cha muda mfupi katika eneo fulani.

Mfano wa magonjwa ya mlipuko ni kama Kipindupindu, UVIKO 19, Ebola, Dengue, Mafua ya ndege  n.k.

Kutokana na tafiti zilizofanywa na wataalamu mbalimbali wa masuala ya afya ndani na nje ya nchi vyanzo vikuu vya magonjwa ya mlipuko huwa ni kutumia maji yasiyo safi na salama yenye vimelea vya bakteria ndani yake, mabadiliko ya majira katika mwaka yaani vipindi vya joto kali au baridi kali, huweza kusababisha mafua makali ambayo huambukiza, kuongezeka kwa ukali wa vimelea wa kuleta ugonjwa mfano kutokea kwa virusi vipya ambavyo watu hawana kinga nayo bado, kufika kwa virusi katika mazingira mapya n.k.

Kufuatia  kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini Tanzania, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia kwa Waziri mwenye dhamana  Mhe. Ummy Mwalimu mnamo tarehe 28 Septemba, 2022 ilitoa taarifa kwa wananchi kupitia vyombo vya habari na kusema kuwa mlipuko wa Ugonjwa huo nchini Uganda unaiweka nchi yetu katika hatari kubwa kutokana na muingiliano mkubwa wa shughuli za kiuchumi na kijamii kupitia mipaka rasmi na isiyo rasmi.

Taarifa hiyo ilifafanua zaidi kuwa Mikoa iliyo hatarini zaidi kupata ugonjwa huo ni Kagera, Mwanza, Kigoma, Geita na Mara. Aidha Mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Songwe, Mbeya na Dodoma ipo katika hatari kwa sababu ya uwepo wa viwanja vya ndege na vituo vikubwa vya mabasi ya kutoka nchi jirani.Hata hivyo, hadi sasa hakuna mgonjwa wa Ebola nchini Tanzania .Hivyo kila mmoja ametakiwa kuchukua tahadhari na kuhakikisha  ugonjwa huo hauingii nchini.

Kutokana na wito huo Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Idara ya Afya imejitahidi kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi juu ya hatua mbalimbali za kuchukua ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko .Mbali na utoaji wa elimu imefanikiwa kujenga jengo au wodi katika eneo la Kipawa ambalo mpaka sasa limegharimu fedha kiasi cha Shilingi Milioni 368 ambayo ni fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji, jengo hilo litaweza kupokea wagonjwa wa magonjwa yote ya mlipuko ikiwepo kipindupindu ,Ebola, UVIKO 19 n.k. endapo watatokea.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambaye ndiye Mkuu wa Idara ya Afya Dkt. Elizabeth Nyema, amesema kuwa kwa sasa jengo hilo lipo tayari kupokea wagonjwa na timu ya wataalamu wamekwishapatiwa mafunzo hivyo wapo tayari kutoa huduma kwa wagonjwa  wakati wowote watakapohitajika.Ameongeza kuwa wao kama wataalamu  wanafanya kazi kwa kushirikiana na watoa huduma ngazi ya Jamii ambapo wataalam hao  wana wajibu wa kutoa elimu na kuhamasisha katika maeneo  yao mara kwa mara lengo likiwa ni kuhakikisha jamii inaelewa nini maana ya magonjwa ya mlipuko, viashiria vya mgonjwa aliyepata maambukizi mapya na njia mbalimbali za kujikinga.

Dkt. Nyema pia ameeleza kwa kifupi kuhusiana na Jiografia ya jengo hilo kuwa litakuwa na uwezo wa kuchukua wagonjwa wapatao 25 ambapo wodi zimetenganishwa kutokana na maelekezo ya kitaalamu ambapo kuna wodi kwa ajili ya wagonjwa ambao ni wahisiwa na wodi ambayo ni kwa ajili wa watu waliothibitika kuwa na maambukizi tayari.

Aidha amebainisha kuwa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam haijaishia hapo katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko. Matarajio yao ni kuendelea kujenga vituo vingine katika maeneo mengine. Mfano ndani ya ramani ya Hospitali ya Wilaya ya Kivule kuna eneo limetengwa kwa ajili ya kujenga jengo la magonjwa ya mlipuko. Hivyo katika bajeti ijayo wanatarajia kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi ya jengo hilo kwa ajili ya wanawake na wanaume kwa sababu eneo la Kipawa lina uwezo wa kupokea wagonjwa wachache. Hivyo wao kama wataalamu wameona lazima wachukue tahadhari ya kuwa na vituo vya ziada endapo watatokea wagonjwa katika kituo cha Kipawa na wakazidi uwezo wa kituo, pawepo na eneo jingine la kuwapeleka.

Wito umetolewa kwa wananchi kuwa na mwitikio chanya pale elimu inapotolewa kuhusiana na magonjwa ya mlipuko. Ili kuepukana na magonjwa hayo jamii imetakiwa kufanya usafi wa mazingira kwa wakati na mara kwa mara. Pia kukusanya na kutupa takataka katika maeneo yaliyotengwai, kunawa mikono wakati wote, sababu maambukizi ya magonjwa ya mlipuko yanaambukizwa kwa kushikana mikono au kukutana na kinyesi au mkojo ambao tayari una maambukizi. Hivyo ili tuwe salama zaidi inatupasa tuchukue tahadhari hizo na tufuate ushauri na maelekezo yote tunayopewa na wataalamu wa afya.

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.