Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Divisheni ya Maendeleo ya Jamii leo Oktoba 11, 2023 wamezindua kampeni ya Habarisha Wanawake, Badilisha Maisha (Inform Women, Transform Lives) yenye lengo la kuhamasisha wanawake kupata habari.
Akisoma taarifa hiyo kwa niaba ya Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa Jiji hilo Bi. Tabu Shaibu ameeleza kuwa “Mheshimiwa Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto ameeleza kuwa tunataka kushirikiana na The Carter Center kwasababu italeta mabadiliko chanya kwa maisha ya kila siku ya Mwanamke katika Jiji la Dar es Salaam huku akisisitiza kuwa taarifa sahihi hutaka maana kubwa kwa wanawake na huwa sauti kubwa ambayo huwa wezesha wanawake kuongeza uelewa katika masuala ya Kiuchumi na kuwapatia fursa katika kuongeza wigo wa kupata huduma za kijamii hivyo kampeni hii haitawasaidia wanawake peke ake bali jamii nzima kwa ujumla wake.”
Aidha Bi. Tabu Shaibu ameendelea kusema Lengo kubwa la kampeni hii ni kuweza kuwafahamisha wanawake haki ya kupata taarifa, kuongeza mitandao ya Kijamii na programu mbalimbali za matangazo kutoka Serikalini pamoja na Taasisi za Serikali kwani makundi mbalimbali ya Wananchi yatawasaidia kuwaunganisha wanawake kupata habari muhimu na kubadilishana mawazo Kutoka katika Miji 35 inayohusika kwenye kampeni hiyo.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Bi. Magreth Mazwile ambaye ndiye mratibu wa Kampeni hiyo amesema “ Kampeni hii ni maalumu kwaajili ya kuhamasisha wanawake kupata habari ilianzishwa na The Carter Center ya Marekani chini ya Rais wa zamani wa Marekani Mhe. Jimmy Carter hivyo kupitia kampeni hii ya ‘Inform Women, Transform LivesCampaign' itawasaidia wanawake kupata habari mbalimbali zinazopatikana katika Halmashauri ikiwemo Habari za Lishe, habari kuhusu mikopo kwa wanawake na habari mbalimbali za kiuchumi zinazotokea nchini, hivyo sisi kama Halmashauri Jiji la Dar es Salaam tutahamasisha wakina mama kupata taarifa kwa njia za redio, televisheni na mitandao ya kijamii.”
Kampeni hii ya awamu ya tatu itakayodumu kwa miaka miwili (2023-2025) imeshirikisha Majiji 12 duniani ikiwemo Dar es Salaam, Tanzania; Accra, Ghana; Baltimore Maryland, Marekani; Glasgow, Scotland; Kathmandu, Nepal; Lagos, Nigeria; Merida, Mexico; Quezon City, Philippines; Quito, Ecuador; Rio de Janeiro, Brazil; Rotterdam, England pamoja na Santiago, Chile.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.