Na: Shalua Mpanda
Halmshauri ya Jiji la Dar es salaam imeibuka mshindi wa kwanza kwa Halmashauri za mkoa huo unaojumuisha halmashauri tano huku ikichukua nafasi ya tatu katika ushindi wa jumla wa Maonesho ya Nanenane mkoani Morogoro.
Halmashauri ya Jiji imekuwa kinara ikiongoza katika halmashauri tano za mkoa wa Dar es salaam huku ikishika nafasi ya tatu katika matokeo ya jumla yaliyoshirikisha halmashauri zote na taasisi zilizoshiriki zinazounda Kanda ya Mashariki.
Maonesho hayo ambayo yamegawanywa kikanda ambapo Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ipo miongoni mwa halmashauri zilizopo katika kanda hii ya Mashariki ikijumuisha mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Morogoro na Tanga.
Akizungumza mara baada ya ushindi huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Elihuruma Mabelya amesema ushindi huo umetokana na ushirikiano uliopo kati ya watumishi na Menejimenti ya Halmashauri hii.
Aidha, amesema ushindi huo utaongeza chachu ya kufanya kazi na kuwaletea wananchi maendeleo.
"Ninawapongeza sana kwa ushindi huu na hii imeonesha namna gani jinsi tulivyo na mshikamano katika utendaji kazi wetu, tuendelee kuwatumikia wananchi ili tumsaidie Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.' Alisema
Maonesho hayo ya wakulima maarufu kama Nanenane yaliyoanaza rasmi Agosti 1,2025 yamefikia tamati leo hii huku Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt. Batilda Burian akiyafunga Maonesho hayo.
“CHAGUA VIONGOZI BORA KWA MAENDELEO ENDELEVU YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI 2025”
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.