Jiji la Dar es Salaam ni miongoni mwa majiji 10 duniani ambayo yamepata tuzo ya C40 Bloomberg Philanthropies 2017 kupitia Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka.
Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka unawahudumia abiria 200,000 kila siku kwa kutumia mabasi ya kisasa ambayo yanachangia kupunguza msongamano wa magari barabarani na kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa na hivyo kuwa siri ya mafanikio ya tuzo hii kwa Jiji la Dar es Salaam.
Tuzo ya C40 Bloomberg Philanthropies hutolewa kila mwaka katika miradi inayotekelezwa kwenye maeneo mahsusi matano ili kutambua jitihada za majiji wanachama wa Taasisi ya mtandao wa Majiji zaidi ya 90 duniani inayoshughulika na namna bora ya kukabiliana na Athari za mabadiliko ya Tabia ya Nchi Duniani “C40 CITIES”.
Mwaka 2017, tuzo hii imetolewa huko jijini Chicago ambapo Jiji la Dar es Salaam limechangia tuzo tajwa na Jiji la New York la nchini Marekani na Jiji la Dar es Salaam liliwakilishwa na Mstahiki Meya wa Jiji, Isaya Mwita Charles.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.