• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Jiji la Dar es Salaam lapongezwa Maonesho ya Nanenane

Posted on: August 1st, 2023

Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Mizengo Kayanza Pinda leo tarehe 1 Agosti, 2023  ametembelea banda la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika Maonesho ya nane nane kanda ya Mashariki yanayojumuisha Mikoa minne ya Tanga, Pwani,Morogoro na Dar es Salaam yanayofanyika mkoani Morogoro katika Viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere kuanzia tarehe 1-8 Agusti, 2023.

Akiwa ndiye Mgeni rasmi wa ufunguzi wa maonesho hayo , Mhe Pinda ameridhishwa na  teknolojia mbalimbali  za Kilimo, Mifugo na Uvuvi nalizooneshwa katika banda la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na kulipongeza Jiji la Dar es salaam kwa maandalizi mazuri yenye ubunifu mkubwa wa teknolojia hizo.

Katika  banda hilo Mhe Pinda ameweza kuona Teknolojia mbalimbali ikiwemo Kilimo cha mbogamboga kwa kutumia Kitalunyumba,utengenezaji wa bustani za nyumbani ( home garden ), teknolojia ya uongezaji wa thamani kwenye mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi, kilimo cha uyoga na mapishi mbalimbali ya uyoga, Ufugaji wa samaki kwenye Mabwawa , Kilimo bila kutumia udongo, Utotoleshaji wa Vifaranga vya Samaki, ufugaji wa kuku , mbwa , ngombe wa maziwa pamoja na kutembelea wajasiriamali  

Aidha  Mhe Pinda pia amepongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kwa kuanzisha maabara maalum ya upimaji wa afya ya udongo ambayo hutumika kufundisha wakulima teknolojia  mbali mbali za kilimo  iloyopo Kinyamwezi katika kata Pugu.

Akitoa shukrani kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala  Mhe  Hashim Komba  ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo amesema kuwa “kwa niaba ya Mhe Edward Mpogolo tunakushukuru sana Mhe Waziri mkuu mstaafu kwa kutembelea banda letu la Halmashauri ya Jiji , Wilaya yetu itaendelea kuwezesha vijana na wanawake ili kuongeza tija kwenye shughuli za kiuchumi wanazofanya”

Aidha Mkuu wa Divisheni  ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Ushirika Ndugu Majaliwa Andrea  kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji ameeleza kuwa  Halmashauri itaendelea kutekeleza sera za Kilimo, mifugo na uvuvi ikiwa ni pamoja na kutenga Asilimi kumi ya mapato ya ndani ya Halmashauri kuwawezesha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kiuchumi.

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.