Mkutano wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabia Nchi ulioandaliwa na taasisi ya Engagement Global ya Ujerumani kwa miji washirika kutoka nchi mbalimbali duniani umeanza leo tarehe 07 Novemba, 2017 alasiri mjini Bonn nchini Ujerumani na utaendelea hadi Novemba 11, mwaka huu.
Jiji la Dar es Salaam linashiriki katika mkutano huo ujumbe wake ukiongozwa na Mstahiki Meya Jiji, Isaya Mwita Charles. Katika ujumbe huo yupo pia Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Bi. Sipora Liana.
Mkutano huo unaofanyika sambamba na Mkutano wa 23 wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia Nchi, COP23 unaihusu miji na taasisi zenye uhusiano na ubia na miji ya Ujerumani katika utekekezaji wa miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi inayofadhiliwa na Ujerumani.
Kutoka Tanzania miji mingine inayoshiriki katika mkutano huo ni Jiji la Mwanza, Manispaa ya Zanzibar na Halmashauri ya Wilaya ya Masasi.
Mstahiki Meya wa Jiji na Mjurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam watashiriki pia katika mkutano wa COP23 ambao Mameya na watendaji wakuu wa majiji na miji mbalimbali duniani watatafuta suluhisho la pamoja la kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi katika miji yao.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita Charles akipokea taarifa ya Maendeleo ya ushirikiano wa miji Dada kati ya Hamburg na Dar es Salaam kutoka kwa Gratz Wolfgang wa Hamburg walipokutana mjini Bonn.
Majiji mawili ya Dar es Salaam na Hamburg yana ushirikiano ulioanza tangu mwaka 2010 ukilenga kushirikiana katika nyanja mbalimbali za maendeleo ambapo katika mkutano huo viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na ujumbe kutoka Mji wa Hamburg walipata fursa ya kujadiliana kuhusu utekelezaji wa mradi wa kuzalisha mbolea zitokanazo na taka za mazao katika Jiji la Dar es Salaam.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.