• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Jiji la Dar lashika nafasi ya sita usafi wa Mazingira Afrika

Posted on: June 2nd, 2022

Jiji la Dar es Salaam limefanikiwa kuwa Jiji la sita kwa kuimarisha usafi wa mazingira ikilingwanishwa na miji mingine ya Afrika. Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Ng’wilabuzu Ludigija, amewaeleza wananchi kuhusu mafanikio hayo katika uzinduzi wa kampeni ya wiki ya mazingira duniani iliyoanza tarehe 02 Juni, 2022. Uzinduzi wa kampeni hiyo, ambayo kilele chake ni tarehe 05 Juni, 2022, umefanyika katika Kata ya Gerezani jijini Dar es Salaam.

 “Kwa hatua hiyo ya mafanikio, wadau wa mazingira mmelipatia heshima Jiji la Dar es Salaam kwa kulifanya kuwa mojawapo kati ya majiji masafi  barani Afrika kwa sababu kwa kutunza mazingira tunakuwa na afya bora na akili timamu inayotusaidia kutekeleza majukumu yetu vizuri, ” alisema Mhe. Ng’wilabuzu.

Mkuu huyo wa Wilaya aliwaelekeza wananchi kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya wiki ya mazingira isemayo “Tanzania moja tu. Tunza mazingira”, akisisitiza utunzaji wa mazingira uambatane na kazi ya upandaji wa miti ili kutimiza lengo la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam la kupanda miti milioni mbili na laki tano.

Mhe.Ludigija ameitumia fursa hiyo pia kuwapongeza wakandarasi wa usafi kwa kazi nzuri wanazozifanya kuimarisha usafi kupitia kampeni hiyo na kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi. Amewataka wakandarasi hao kuendelea na kazi zao bila kuchoka kwa kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ni taswira ya Tanzania kwa usafi.

Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omari Kumbilamoto, amempongeza  Mkuu wa Idara ya Mazingira katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Rajabu Ngoda kwa kazi nzuri ya kuliweka Jiji safi kupitia Idara ya Mazingira.

Aidha, Mstahiki Meya amemuomba Mkuu wa Wilaya kuzifikisha salamu za wananchi wa Dar es Salaam kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwamba kwa takribani miaka sasa Jiji la Dar es Salaam halijawa na changamoto za magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu.

Katika uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Jumanne Shauri, naye aliwaambia wananchi kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imejipanga kufanya operesheni ya usafi kwa kuzingatia kwamba Jiji hilo ni kitovu cha shughuli nyingi. “Usafi unaanza na mimi. Timiza wajibu wako”, alisema Shauri akiahidi kuendeleza juhudi za kuimarisha usafi.

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.