Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inakusudia kuwafikia wakazi zaidi ya Milioni Moja ambao watapata dawakinga kwa ajili ya kudhibiti ugonjwa wa Matende na mabusha katika Kata 36 na mitaa 256 ya Jiji Hilo. Hayo yamebainishwa leo Novemba 18, 2022 katika kikao kazi cha mpango wa kutoa dawa kinga kwa ajili ya kudhibiti ugonjwa wa matende na Mabusha kilichofanyika katika ukumbi wa Mganga Mkuu wa Jiji la Dar es Salaam.
Kikao hicho kilichohudhuriwa na wataalamu mbalimbali kutoka Wizara ya Afya kililenga kutoa elimu kwa Madaktari wa Jiji la Dar es Salaam ili waweze kuanza kampeni ya kutoa chanjo hiyo mapema kwa Wananchi wa Jiji hilo.
Akiongea kwenye kikao kazi cha mpango wa kuanza kutoa dawakinga Kwa ajili ya kudhibiti ugonjwa wa Matende na mabusha Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Bibi. Charangwa Selemamn amesema Ilala itawafikia zaidi ya Wakazi Milioni 1.2 katika zoezi litakaloanza Novemba 21-25 mwaka huu.
“Niwatoe wasiwasi wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kuwa chanjo hii haina madhara yoyote hivyo msiogope kujitokeza kupata dawa kinga kwaajili ya magonjwa haya hivyo nitoe wito kwa wananchi wa kata zote na mitaa yote na Jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kupata dawa hizo ili tuweze kupunguza madhara yatakayokuja kujitokeza badae". Amesema Bibi Charangwa .
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Jiji la Dar es Salaam Dr. Elizabeth Nyema amesema dawakinga hizo hazina madhara hivyo amewasihi wakazi wa Ilala kuhakikisha wanameza dawa hizo ili kuzuia matende na mabusha.
"Niwahakikishie tuu mtakua salama kwanj dawa hizi hazina madharayoyote na hata hivyo dawakinga hizo zitatolewa Kwa wenye umri kuanzia miaka mitano na kuendelea ila hazitatolewa Kwa wanawake wajawazito pia Kwa kina mama wanaonyonyesha."
Sambamba na hilo Dr. Nyema ameendelea kusema ugonjwa wa matende na mabusha husababishwa na mbu hivyo tutatoa dawakinga hizo kwa kupita nyumba kwa nyumba, maeneo ya stendi pamoja na shule takribani 110 pia tutatoa elimu kwa walimu 110 ili waweze kuwaelimisha wanafunzi waweze kupata kinga hiyo.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.