Katika kuhakikisha Wananchi Wanapata huduma kwa Ukaribu zaidi Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imenunua Bajaji 35 na Pikipiki 7 zitakazogawanywa katika Kanda saba za kutolea huduma ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambazo zimekabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala leo Oktoba 19, 2023 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini humo.
Akikabidhi Vyombo hivyo Mhe. Mpogolo amesema “Kuanzishwa kwa Kanda saba za huduma kumeleta mafanikio makubwa kwani makusanyo ambayo yamekua yakikusanywa yameweza kununua bajaji na pikipiki zitakazo rahisisha usafiri wakati wa kwenda kukusanya mapato na kufuatilia vibali vya ujenzi hivyo nimpongeze Mkurugenzi wa Jiji kwa kuanzisha Kanda hizi za huduma kwani huduma zimewafikia Wananchi kwa ukaribu na mapato yamekua yakikusanywa zaidi. Hata hivyo kutokana na bajaji na pikipiki hizi ambazo tunazikabidhi hapa ni imani yangu Watendaji watapata motisha ya kukusanya mapato zaidi kwakuwa wamerahisishiwa huduma za usafiri kwa ajili ya kuwafikia wananchi kwa ukatibu zaidi, pia nipende kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri anayoifanya ya kujenga uchumi wa nchi yetu hivyo juhudi zetu hizi ni kwaajili ya kumuunga mkono Rais kwa kuhakikisha Wananchi wanapata huduma stahiki kwa wakati na kwa ukaribu zaidi.”
Naye Mstahiki Meya Wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Omary Kumbilamoto ameweza kusema “Uwepo wa bajaji hizi na pikipiki zitazalisha ajira mpya kwani madereva 35 watahitajika pia kutokana na bajajai hizi huduma zitarahisishwa na wananchi watafikiwa kwa uharaka zaidi na mapato yatakusanywa kwa kasi zaidi.”
Awali akiongea katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Ndg. Jomaary Satura ameeleza kuwa “Bajaji hizi na pikipiki zimenunuliwa kwa fedha za mapato ya ndani takribani shilingi Milioni 312.3 hii ikiwa ni mpango mkakati wa mwendelezo wa kuboresha Kanda zetu za huduma kwani katika kila Kanda tutatoa bajaji 5 na pikipiki moja hii itawasogezea wananchi huduma na tutaendelea kuzijengea Kanda zetu uwezo awamu kwa awamu kwani adhma yetu ni kuwahudumia wananchi kwa uadilifu mkubwa pamoja kukusanya mapato na kuyatumia kwa uadilifu mkubwa ili kutimiza adhma ya Rais wetu ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kwa ukaribu zaidi.”
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.