Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Tabu Shaibu ameahidi kushirikiana na Jiji la Hamburg katika kuboresha bustani ya Mimea inayopatikana mtaa wa Luthuli katika Kata ya Kivukoni Jijini Dar es Salaam.
Bi. Tabu Shaibu ameyasema hayo leo Disemba Mosi, 2023 wakati wa hafla ya siku ya watu iliyoandaliwa na Jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na Jiji laHamburg yenye lengo la kutoa mrejesho kwa wananchi na wadau wa maendeleo kuhusu kilicho had ukiwa katika warsha ya siku sita ya jinsi ya kuboresha bustani ya mimea ili waweze kutoa mawazo yao kuhusu uboreshaji wa bustani hiyo.
Akiendelea kuongea katika hafla hiyo Bi. Tabu Shaibu amesema "Nipende kuwashukuru wenzetu kutoka ujerumani kwani siku tano wameonesha msimamo wao na mchango wao mkubwa katika kutekeleza mradi huu hivyo niwaahidi yote yaliyojadiliwa yanaingia kwenye kumbukumbu za utekelezaji kwasababu tayari Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam tumetenga fedha kwaajili ya uboreshaji wa bustani yetu hivyo nitoe wito kwa kila mmoja atakayepewa majukumu kuyasimamia vizuri pia niwahakikishie uhusiano huu utadumi na kila mmoja atajifunza kutoka kwetu.”
Kwa upande wake Kansela wa Seneti wa Jiji laHamburg ambaye ni Mkurugenzi wa Maendeleo na Ushirikiano wa Miji Dada na Dar es Salaam Dr. Anna Catarina Cebode ameeleza kuwa “Tumekua na wiki ya mafanikio kwani siku tano za warsha zimetufanya tubadilishane mawazo na uzoefu na pia tumeona ukarimu wenu hivyo nitoe wito kwa wananchi kushirikiana na vikundi vyetu ili kutoa mawazo chanya yatakayosaidia kuboresha bustani yetu ya mimea.”
Aidha katika kutekeleza mradi huu kutakua na vikundi kazi vinne ambavyo vitawezesha ukamilishaji wa Bustani ya mimea, vikundi hivyo ni pamoja na kikundi cha kuvuna maji, kikundi cha uhifadhi wa mimea, kikundi cha historia na urithi pamoja na kikundi cha elimu, matukio na mgahawa ambapo vikundi hivi vitakua na mchango mkubwa katika kuhakikisha bustani yetu inakua imara kiutalii,elimu na biashara.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.