Katika kilele cha maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo tarehe 9 Desemba, 2024 limepanda miti katika fukwe za dengu na kufanya usafi wa mazingira katika soko la Ilala na Buguruni.
Akiongea na wananchi na wadau malimbali waliojitokeza katika Zoezi hilo, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Ndg. Elihuruma Mabelya Amesema “Nia ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona mazingira ya nchi yanakuwa safi na salama hivyo na sisi Jiji la Dar es Salaam tumejipanga vyema kuhakikisha suala la utunzaji wa mazingira tunalipa kipaumbele na linakua endelevu ili kuhakikisha tunapendezesha Jiji na wananchi wetu wanaishi na kufanya biashara katika mazingira safi na salama kwa mustakabali wa Afya zao."
Sambamba na hilo, Ndg. Mabelya amewashukuru wadau malimbali wa Mazingira na wananchi waliojitokeza kuhakikisha zoezi la usafi linafanyika na amewahakikishia kuwapa ushirikiano katika kutunza Mazingira ya Jiji la Dar es Salaam.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.