Na: Shalua Mpanda
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mheshimiwa Balozi Omar Ramadhan Mapuri leo hii Mei 21,2025 amefanya ziara kukagua zoezi la uboreshaji na uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam.
Mhe.Balozi Mapuri katika ziara hiyo ambayo aliambatana na Afisa Mwandikishaji wa Jiji la Dsm Wakili Faraja Nakua ameweza kutembelea vituo vya Halmashauri ya Jiji,Liwiti,Mchafukoge na Ukonga huku akionekana kuridhishwa na zoezi hilo kwa jinsi linavyoendelea.
Aidha, Balozi Mapuri amesisitiza wananchi kuendelea kujitokeza katika vituo hivyo na kutumia siku moja tu iliyobaki kuhakiki taarifa zao na kutoa wito kwa wale ambao bado hawajajiandikisha kutumia muda huu kufanya hivyo ili wawe na sifa ya kupiga kura ifikapo Oktoba mwaka huu.
"Nawaombeni muendelee kujitokeza na kuwafahanisha wale wengine ambao bado kutumia fursa hii kabla ya zoezi hili kuhitimishwa hapo kesho". Alisisitiza
Kabla ya kuanza ziara hiyo Mjumbe huyo wa Tume Huru ya Uchaguzi alipata fursa ya kutembelea ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji na kufanya mazungumzo mafupi na Mkurugenzi wa Jiji hili Ndugu Elihuruma Mabelya amemtembelea ofisini kwake Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salama, Ndugu. Elihuruma Mabelya.
Zoezi hili ambalo lilianza Mei 16,2025 ni la awamu ya pili mara baada ya lile la kwanza ambapo linatarajiwa kukamilika kesho Mei 22,2025 hivyo Wananchi hawana budi kujitokeza kushiriki zoezi hili litakalowawezesha kuchagua viongozi wanaowataka kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.