• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Kamati ya Kudhibiti UKIMWI Jiji la Dar es Salaam yatembelea Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo kukagua Shughuli wanazozifanya katika kupambana na Maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI

Posted on: October 26th, 2023

Kamati ya Kudhibiti UKIMWI ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, leo tarehe 26 Oktoba, 2023 wamefanya ziara ya kutembelea na kukagua shughuli zinazofanywa na Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo iliyopo Kata ya Gongolamboto Mtaa wa Ulongoni yenye lengo la kuhamasisha jamii kwa kusaidia na kuwajengea uwezo watoto, wanawake na vijana waishio katika mazingira magumu pamoja na watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI (WAVIU) ili waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali za kimaisha.

Akiongea wakati wa ziara hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudhibiti UKIMWI Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mjumbe wa Kamati hiyo Mhe. Lucy Lugome amesema “Nipende kuwashukuru sana Taasisi ya Fahari kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kusaidia jamii ya watu wa makundi maalumu hadi kutupelekea Leo hii kuja kukagua miradi yenu japo ni sehemu ya majukumu yetu lakini pia kutambua mchango wenu kama Taasisi katika kutoa Elimu kwa Umma juu ya kudhibiti maambukizi mapya ya VVU na UKIMWI hivyo ziara hii ni sehemu ya utekelezaji wa miradi pamoja na kuhakikisha huduma zote zinazotolewa kwa WAVIU zinatekelezwa katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa Fedha 2023/2024 ulioanza Julai hadi Septemba 2023."

Aidha Mhe. Lugome ameendelea kusema “Ziara yetu imekua na mafanikio zaidi kwani tumeweza kujifunza shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Taasisi ya Fahari ambayo imekua na mchango mkubwa wa kutoa lishe kwa WAVIU kwa lengo la kuimarisha Afya zao lakini pia mbali na kufanya shughuli hizo kwa weledi napende kutoa wito kuhakikisha wanatafuta Mtaalamu Afya atakaeweza kuwaelekeza watu hao namna gani ya kutumia dawa kama inavyoelekezwa.” 

Sambamba na hilo Mhe. Lugome ametoa wito kwa Asasi nyingine pamoja na wadau wengine kuiga mfano wa Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo huku akiwataka Maafisa wa Ustawi kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kushirikiana na Shirika hilo ili kuweza kupunguza changamoto za watoto wanaoishi katika mazingira magumu ndani ya Jiji la Dar es Salaam.

Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Shirika kwa kipindi cha Mwaka 2019-2023 Mkurugenzi wa Shirika hilo Bi. Neema Mchau ameeleza kuwa Shirika la Fahari tuamke maendeleo ni Asasi iliyoanzishwa na kusajiliwa mwaka 2016 chiniya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wanawake na makundi Maalumu ikiwa na lengo la kuanzisha jamii yenye maisha bora na ustawi kupitia ujasiriamali, haki za watoto, hifadhi za mazingira pamoja na uwezeshaji wananchi Kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

Sambamba na hilo Bi. Mchau ameeleza kuwa "Shirika la Fahari Tuamke Maendeleo linajishughulisha na kutoa elimu juu ya umuhimu wa matumizi sahihi ya dawa pamona na kuwapa vyakula na lishe watu waishio na maambukizi ya virusi vya Ukimwi (WAVIU) ambapo hadi kufikia sasa tumeweza kuwafikia WAVIU 20 walioko Kata ya Majohe pia tumekua tukihamasisha utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwa kushirikiana na jamii katika kupanda miti ya matunda na vivuli kwenye Taasisi za Serikali ikiwemo Shule za Msingi Bangulo na Ushindi pamoja na Zahanati ya Yongwe na Kituo cha Afya Chanika hivyo nipende kutoa Shukrani zangu kwa wajumbe wote kwa kututembelea leo naahidi ushirikiano naninyi katika kuhakikisha tunatatua changamoto zote zinazohusiana na watoto wa mazingira magumu pamoja na WAVIU wote kwa ustawi wa Jiji letu na Nchi kwa ujumla."

Aidha Kamati imeagiza wataalamu wa afya kuwajengea uwezo Fahari Tuamke Maendeleo wakati wanapotoa huduma kwa WAVIU pamoja na kuwaeleza namna ya kuwa na  usiri wakati  wanapofanya shughuli za kuhudumia makundi maalumu huku wakiwataka wataalamu hao kufuatilia takwimu za Waviu kwa Fahari Tuamke Maendeleo ili kujua kama wanapatikana kwenye Konga ni wapya.

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.