Na; Judith Msuya
Kamati ya Siasa Wilaya ya Ilala leo August 30, 2021 wamefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kipindi cha January hadi Juni 2021ili kuweza kuangalia utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) 202-2025.
Wakiwa kwenye ziara hiyo, Kamati iliweza kutembelea na kukagua Miradi Sita ikiwemo; ujenzi wa vyumba vya Madarasa Manne (4) pamoja na umaliziaji wa ukarabati wa Maabara Tatu (3) za Sayansi katika shule ya Sekondari Mivinjeni ambapo Mradi huo umetumia kiasi cha shilingi Milioni 79.9 na mpaka sasa Mradi wa Vyumba vya Madarasa Manne (4) umekamilika na wanafunzi wapo Madarasani huku Mradi wa umaliziaji wa Maabara ambao ukikamilika utagharimu takribani Shillingi Milioni 100.7 na ujenzi unaendelea kutekelezwa.
Mradi mwengine uliotembelewa na kamati hiyo ni ujenzi wa Madarasa Matano (5) na Maabara Mbili (2) za Sayansi katika shule ya Sekondari Kinyerezi Annex ambapo Mradi huo uliogharimu takribani Shilingi Milioni 100 umekamilika huku mradi wa maabara ya Physics na Biology wenye gharama ya Shilingi Milioni 60 ukiwa umefikia asilimia 98 ili kukamilika pamoja Mradi wa ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa katika shule ya Sekondari Kitunda ambao ushakamilika na madarasa yakiwa yanatumika.
Sambamba na hilo Kamati iliweza kukagua ujenzi unaoendelea katika Barabara ya Ulongoni ‘A’ na ‘B’, Stendi Mpya ya Kinyerezi pamoja na ujenzi wa barabara ya Amani na Likoma zilizopo kata ya Kariakoo.
Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala Ndug. Abdul-Azizi Ubaya Chuma akifanya majumuisho ya ziara hiyo amesema "kimsingi kwa utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi pamoja na matumizi ya fedha tumeweza kujiridhisha kwamba Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wameweza kusimamia vizuri miradi hii lakini ombi letu tunawaombaa waendelee kusimamia miradi hii na waweze kutatua kero ndogondogo zinazokwamisha kukamilika kwa mradi mfano katika barabara ya kilometa 7.5 ya Kinyerezi kuna mwingiliano kati ya Shirika la Reli Tanzania na bomba la mafuta TAZAMA hivyo tunawaomba Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala waweze kutatua kero hiyo ili barabara hii isikwame na ikamilike kwa wakati”
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.