Kamati ya siasa Wilaya ya Ilala leo tarehe 2 Disemba 2022 imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Ilani ya Chama cha Mapinduzi, kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Ndg. Saidi Side pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Ngwilabuzu Ludigija ambapo wameweza kutembelea ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Kamati ya Siasa imeridhishwa na utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi katika ngazi ya ujenzi wa madarasa ya mradi wa "Pochi ya Mama" katika Wilaya ya Ilala. Ndg. Side amesema "Tunamshukuru Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi cha Shilingi Bilioni 6 katika Wilaya ya Ilala kwa ajili ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa. SIsi kamati ya Siasa tumetembelea ujenzi huu wa madarasa tumeridhishwa mpaka sasa asilimia 80% ya kazi iliyofanyika ni kazi bora na nzuri sanaa umezingazia viwango tunawapongeza pia maafisa wote, walimu, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi na wengine kwenye kuimarisha usimamizi"
Akiendelea kusema kuwa changamoto zilizopo ni ndogo kuelekea mwezi wa kwanza kuweza kukamilisha ili wanafunzi watakao chaguliwa kuingia kidato cha kwanza waweze kupata elimu kwa wakati.
Aidha, mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala ameeleza kwamba kwa shule zote ambazo ujenzi unasua sua waimarishe nguvu ili wakamilishe kwa wakati pia wote ambao wamefanya vizuri katika kutekeleza ujenzi huu basi wapewe motisha.
"Mimi na kamati yangu ya siasa pamoja na wajumbe wote wa CCM Wilaya tumejifunza vingi sana katika ziara hii nawapongeza sana wajumbe kwa kujitoa vile vile Mkurugenzi aweke uangalizi kwa wote wanaofanya vizuri katika ujenzi huu wapewe motisha na wote wanaofanya vibaya hawana budi kutembelea na kujifunza kwa wenzao"
Vilevile Mkuu wa Wilaya ya Ilala amekiri kuona kazi inayofanywa na kamati ya Siasa katika ukaguzi wa miradi ikiwa ni sehemu ya utekelezwaji wa ilani ya CCM akiwa ameongozana na kamati hiyo amesema "Ninakiri kuwa kamati ya Siasa Wilaya ipo vizuri na nitatoa maagizo katika kuzidi kufuatilia ufanyaji wa kazi usiku na mchana ili ujenzi huu umalizike kwa wakati kabla ya mwezi wa kwanza"
Akiwa katika Majuhisho ya ziara hiyo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano Anatoglou Mnazi Mmoja Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Ndugu Side ameeleza kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Idara ya maendeleo ya Jamii katika utoaji wa mkopo wa asilimia kumi kwa vijana, wanawake na watu wenye Ulemavu.
"Sisi kama kamati ya Siasa tunaahidi kuunga mkono na tutafuatilia kwa kiasi kikubwa urejeshaji wa mikop hii kutoka kwa vikundi vyote na tutaanza vile vya vijana wa CCM"
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.