Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala chini ya Mwenyekiti wake Ndg. Said Sidde leo Februari 7, 2024 imefanya ziara ukaguzi wa miradi ya maendeleo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchagu.
Miradi iliyotembelewa na Kamati hiyo ni pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Mchikichini wenye gharama ya shilingi Bilioni 5, Kituo cha Afya Kinyerezi kinachojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 500, Ujenzi wa barabara ya Pugu-Majohe yenye urefu wa mita 400 wenye thamani ya milioni 140 fedha kutoka mapato ya Ndani ya Halmashauri, Ujenzi wa ghorofa 4 Shule ya Sekondari Minazi Mirefu uliogharimu shilingi milioni 870 na mradi wa madarasa shule ya msingi mizengo wenye thamani ya milioni 100.
Akiongea wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Ndg. Said Sidde amesema “Naipongeza sana Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wakiongozwa na Mstahiki Meya na Mkurugenzi kwa utekelezaji wa miradi kwani thamani ya fedha inaonekana pia miradi inatekelezwa kwa kiwango cha juu. Hii inaonyesha ni jinsi gani Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inavyotekelezwa kwa kasi hivyo niwaombe kukamilisha miradi ya zamani kwa wakati na miradi mipya iendelee na ikamilike kwa wakati.”
Awali akiwasilisha taarifa ya miradi na utekelezaji wa Ilani kwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Ilala, Mkuu wa Wilaya ya hiyo Mhe. Edward Mpogolo ameeleza kuwa “Viongozi tuna deni kwa Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, kwa sababu fedha zote zilishatolewa. Hivyo ni matumaini yake kuona miradi yote katika sekta za Elimu, Afya, na Barabara inakamilika kwa wakati. Hivyo nitoe wito kwa wasimamizi wa miradi kujituma na kufanya kazi kwa bidii ili kukamilisha miradi kwa manufaa ya wananchi wa Ilala na maeneo ya jirani."
Aidha Mhe. Mpogolo ameendelea kusema kuwa “Halmashauri yetu katika jitihada za kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Jiji la Dar es Salaam tumeweza kuanzisha Kanda za huduma 7 ambazo zinasaidia wananchi kupata huduma kwa ukaribu zaidi ikiwemo vibali vya ujenzi pamoja na huduma nyingine muhimu ambapo baada ya kuanzishwa kwa Kanda hizo ongezeko la ukusanyaji wa mapato limeongezeka na wananchi wanapata huduma kwa ukaribu." Amesema.
Kwa upande Mstahiki Meya Mhe. Omary Kumbilamoto amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala kwa ziara aliyoifanya huku akimuhakikishia kutekeleza maelekezo yote aliyoyatoa kwa manufaa ya wananchi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.