• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii Jiji la DSM yakagua Miradi ya Maendeleo iliyotekelezwa kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai - Septemba, 2023

Posted on: October 24th, 2023

Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, leo tarehe 24 Oktoba , 2023 wamefanya ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo iliyotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kipindi cha robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 (Julai hadi Septemba 2023.)

Wakiwa kwenye ziara hiyo, Kamati iliweza kutembelea na kukagua miradi minne (4) ikiwemo ujenzi wa Madarasa ya ghorofa Shule ya Sekondari Mnazi Mmoja, ujenzi wa uwanja wa Mpira Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa, ujenzi wa Madarasa 8 na matundu 13 ya Vyoo Shule ya Sekondari Jangwani pamoja na ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi Boma.

Aidha, ujenzi wa  madarasa 20 ya ghorofa 4 Shule ya Sekondari Mnazi Mmoja mmoja uliogharimu takribani shilingi Milioni 540 ikiwa kwenye hatua ya Frame work na hadi kukamilika utagharimu shilingi bilioni 1.8, Ujenzi wa Madarasa 8 na Matundu 13 ya Vyoo Shule ya Sekondari Jangwani yenye thamani ya shilingi milioni 199.4 Fedha kutoka kwa wafadhili Barrick Gold Mine ikiwa mchango wao wa kurudisha hisani kwa jamii mbapo Madarasa nane (8) yaliyogharimu shilingi milioni 176 yakiwa yamekamilika huku matundu 13 ya vyoo yenye thamani ya shilingi  milioni 23.4 yakiwa katika hatua ya ukamilishaji pia ujenzi wa Shule ya Msingi Boma Mpya yenye madarsa sita (6) ya Msingi na Madarasa mawili (2) ya awali, jengo moja (1) la utawala na matundu kumi na sita (16) ya vyoo uliogharimu shilingi milioni 306.9 Fedha kutoka Mradi wa Boost ukiwa umekamilika huku ujenzi wa uwanja wa mpira Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa unaotekelezwa kwa Fedha za Mapato ya Ndani ya Halmashauri ukiwa umefikia asilimia 35% ya utekelezaji ambapo hadi kufikia Disemba 31, 2023 mradi huo utakuwa umekamilika na utagharimu shilingi milioni 989.8.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Saady Khimji akifanya majumuisho ya ziara hiyo amesema, "Leo tumetembelea baadhi ya miradi inayosimamiwa na kutekelezwa na Halmashauri ya Jiji la DSM ambapo tumeweza kuridhishwa na utekelezaji huo hivyo nitoe wito kwa watendaji wa Halmashauri kusimamia miradi hii kwa ukaribu zaidi na Sisi kama wasimamizi tutaendelea kushirikiana nao kuhakikisha miradi hii inatekelezwa kwa wakati na thamani ya Fedha inayotumika inalingana na ubora wa miradi."

Sambamba na hilo Mhe. Khimji ameendelea kusema, "Kamati hufanya ziara hizi kwa lengo la kukagua na kuhakikisha fedha zinazotolewa na Serikali Kuu pamoja na Halmashauri zinawafikia walengwa na kufanya kazi kama ambavyo wao wamepitisha kupitia vikao vya Madiwani na kuangalia thamani ya fedha hizo na kazi zinazofanyika hivyo naomba mapungufu yaliyoonekana kwenye miradi hiyo yashughulikiwe kwa wakati na kuweza kufikia hitimisho sahihi kwani tunachohitaji wananchi wote wafikiwe na huduma muhimu na bora kwa wakati kama Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania anavyoonesha juhudi zake katika kuwahudumia Wananchi.”

Aidha, Wajumbe wa Kamati wameridhia kuwa endapo kutakua na changamoto wakati wa utekelezaji wa miradi ni vyema changamoto hizo zikawasilishwa sehemu husika mapema na kufanyiwa kazi ili maendeleo ya wananchi yasikwamishwe huku wakiagiza miradi yote ya madarasa ya Boost yatembelewe ili kukagua kama kuna changamoto na zifanyiwe marekebisho kabla madarasa hayo hayajaanza kutumika.

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.