Kamati ya Uwekezaji, Biashara na Viwanda ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, leo Novemba 4, 2024 imefanya Ziara ya ukaguzi wa maeneo yanayotarajiwa kufanyiwa Uwekezaji yanayosimamiwa na Jiji la Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo, Kamati imetembelea na kukagua kiwanja kilichopo maeneo ya Oysterbay chenye ukubwa wa mita za mraba 5940 pamoja na kiwanja cha wazi cha Mkunguni chenye ukubwa wa mita za mraba 3240.
Akiongea katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Ojambi Masaburi amesema “Kamati hii ni mahususi kwa kubainisha maeneo ambayo ni fursa na vitega uchumi vya Halmashauri, kwani Halmashauri yetu ina maeneo mengi na makubwa ambayo tukiyatumia vizuri katika uwekezaji yatasaidia kuingiza mapato katika Halmashauri yetu ambayo yatasaidia kuboresha miundombinu katika secta ya Afya, Elimu, na miundo mbinu ya barabara”
Sambamba na hayo, Mhe. Masaburi amesema Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam inawakaribisha Wawekezaji wa ndani na nje ya Nchi kuja kuwekeza katika Jiji la Dar es salaam kwani kuna maeneo mengi na makubwa na mazuri yanayofaa katika Uwekezaji.
Aidha, Kamati imeagiza Halmashauri kubainisha maeneo yote ambayo yanatarajiwa kufanyiwa uwekezaji Ili Kamati iweze kupendekeza vitega uchumi vitakavyokua na maslahi kwa Halmashauri na Taifa kwa ujumla.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.