Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaaa (OR-TAMISEMI) kupitia Kitengo cha Uratibu wa Miradi ya Mikopo Nafuu kutoka Benki ya Dunia leo tarehe 06 Juni, 2023 Katika Ukumbi wa Mikutano Arnatouglou Jijini Dar es Salaam wamefanya kikao kazi na Madiwani, Wadau pamoja na Wakuu wa Idara kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya Mradi wa uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam awamu ya pili (Dar es Salaam Metropolitan Development Project – DMDP Phase 2).
Akiongea Katika Kikao hicho Afisa Mazingira naMasuala ya Kijamii Bi. Agness Akatukiza Kishenyi amesema “Lengo la Kikao hichi kwa Waheshimiwa Madiwani pamoja na Watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ni Kutambulisha mradi wa DMDP awamu ya pili pamoja na kupata maoni yenu kuhusiana na mapendekezo ya mradi wa DMDP awamu ya pili kwaajili ya maandalizi ya Nyaraka za Kimazingira na Masuala ya Kijamii (Environment and Social Management Framework and Ressetment Policy Framework (ESMF & RPF)."
Sambamba na hilo Bi. Agness ameeleza kuwa mapendekezo ya Barabara DMDP awamu ya pili zimegawanywa katika asilimia 100%, 70% pamoja na Asilimia 30% ambapo katika mapendekezo ya Barabara DMDP awamu ya Pili Asilimia 30% zinaweza kufanyiwa marekebisho Kulingana na Mapendekezo ya Waheshimiwa Madiwani.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Eng. Amani Mafuru ameeleza kuwa kutekelezwa kwa miradi hii itaibadilisha sura ya Jiji la Dar es Salaam na kutoa muonekano ambao Mhe. Rais ameendelea kutilia msisitizo uwepo wa Miji nadhifu iliyopangwa na yenye mandhari nzuri, hivyo natoa wito kwa Waheshimiwa Madiwani kuwa Sisi Kama Halmashauri tutaendelea kutenga fedha ili kuweza kuboresha maeneo ambayo hayatafikwa na mradi huu wa DMDP awamu ya pili.
Akifunga Kikao hicho Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mhe. Ojambi Masaburi ametoa shukrani zake za dhati kwa mapendekezo ya Barabara DMDP awamu ya pili huku akiazimia kuwa barabara za DMDP awamu ya pili asilimia 30% zifanyiwe marekebisho kama Waheshimiwa Madiwani walivyopendekeza.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.