• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo kuzalisha ajira 20,000

Posted on: September 29th, 2017

MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amekutana na ugeni kutoka Jiji la Shanghai nchini China na kujadili mambo mbalimbali ya maendeleo jijini hapa ikiwemo suala la uboreshaji wa Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Mikoani na nchi jirani cha Ubungo.

Ugeni huo ulioambatana na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Linghang, Cathy Wang ambayo ndiyo imeingia mkataba na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo hayo, Meya Mwita alisema kuwa ugeni huo umeridhia kuwekeza katika nyanja mbalimbali ikiwemo Kituo cha Mabasi Ubungo.

Alifafanua kuwa Jiji la Dar es Salaam linakaribia kuanza kufanya ujenzi wa mradi mkubwa wa kubadilisha Kituo cha Mabasi Ubungo na kwamba hatua mbalimbali zimeshakamilika ili kupisha mradi huo.

Alisema kuwa mara baada ya kukamilika kwa mradi huo jumla ya Watanzania 20,000 watapata ajira jambo ambalo litawezesha kuongeza kipato kwa wananchi na hivyo pia kuwawezesha vijana kuondokana na makundi ambayo sio salama.

Alisema kufanikisha kwa mradi huo, kutasaidia pia kuongeza mzunguko wa fedha jijini hapa kutokana na kuwepo kwa fursa nyingi za kibiashara.

“Leo nimekutana na ugeni ambapo kwa kiasi kikubwa mnafahamu ndugu zetu hawa wamekuwa na urafiki mkubwa na nchi yetu, tumejadiliana mambo mengi ambayo yote ni kwa lengo la kuleta maendeleo katika Jiji letu.

“Lakini kubwa zaidi ni kuhusu ujenzi wa Kituo cha Mabasi Ubungo, ambapo hivi karibuni tunatarajia kuanza kwa mradi huo, na wananchi pia watajulishwa, nitumie fursa hii kuwaeleza wananchi kuwa Jiji linafuata utaratibu katika kutekeleza mradi huo” alisema Meya Mwita.

“Fursa hii kubwa ambayo tumeipata, Watanzania watapata ajira, mzunguko wa fedha kwenye Jiji letu utaongezeka, kama Meya wa Jiji hili nimewakaribisha tufanye kazi pamoja, lengo likiwa nikuweka Jiji kwenye muonekano mzuri” aliongeza.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kampuni ya Linghang, Cathy Wang alimpongeza Meya Mwita kutokana na aina ya utendaji wake wa kazi na kuahidi kuonyesha ushirikiano katika utekelezaji wa mradi huo.

Alisema kuwa Meya Mwita ni kiongozi anayefanya kazi kwa bidii na umakini na kwamba kutokana na jitihada hizo za kulijenga Jiji, kampuni yao itafanya  kazi kwa ushirikiano mkubwa.

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.