Katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Mashujaa, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Kitengo cha Udhibiti Taka Ngumu na Usafishaji pamoja na Kitengo cha maliasili na uhifadhi wa Mazingira leo Julai 24, 2024 wamefanya usafi wa mazingira katika eneo la Soko la Kimataifa la Samaki Feri na Stendi ya Kivukoni ikiwa ni sehemu ya kuwaenzi mashujaa waliopoteza maisha yao katika kutetea na kulinda Uhuru wa Tanzania.
Akizungumza katika zoezi hilo, Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Taka Ngumu na Usafishaji Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bw. Rajabu Ngoda ameeleza kuwa “Katika kuelekea Kilsisi kama Halmashauri ya Jiji tumewakumbuka mashujaa wetu kwa kufanya usafi katika maeneo haya ya Kivukoni hivyo niwahimize Wananchi, wafanyabiashara na wadau mbalimbali wa mazingira kuhakikisha mnafanya usafi wa kila siku katika maeneo bila kushurutishwa lengo likiwa ni kuweka mazingira ya Jiji la Dar es Salaam katika hali ya usafi lakini pia kuepuka na magonjwa ya mlipuko”.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira Jiji la Dar es Salaam Bi. Theresia Denis ameeleza kuwa mbali na kuwakumbuka Mashujaa waliopigania Uhuru pia usafi huo umekua ni sehemu ya kuwakumbusha Wananchi kutunza mazingira ya Jiji kwaajili ya afya ya Jamii huku akiwahimiza kufanya usafi kuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku na sio kusubiri matukio maalumu.
Naye Meneja wa Soko la Kimataifa la Samaki Feri ametoa wito kwa Wafanyabiashara wa Soko hilo kuhakikisha wanatunza mazingira kwa kuyaweka katika hali ya usafi kabla na baada ya kumaliza biashara zao.
Aidha Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa huadhimishwa kila tarehe 25 Julai ya kila Mwaka.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.