Meya wa Jiji la Dallas, Texas, Eric L. Johnson, kwa kushirikiana na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto, wamesaini makubaliano ya kuwa Majiji Dada (Sister City Partnership) kati ya Dallas na Dar es Salaam. Makubaliano hayo yanalenga kuimarisha ushirikiano katika maeneo ya biashara, elimu, utamaduni na maendeleo ya jamii.
Hafla ya utiaji saini ilifanyika Leo tarehe 22 Julai 2025, katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Jonathan Howard, na maafisa waandamizi kutoka Serikalini pamoja na sekta binafsi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.