• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Mashehe wa Jiji la Dar es Salaam wampongeza Meya Mwita kwa kuwakutanisha waumini wa Kiislam kwenye futari

Posted on: June 17th, 2017

MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita jana aliwafuturisha wakazi wa Jiji la Dar es Salaam zaidi ya 600 kutoka sehemu mbalimbali  jijini hapa nakutumia nafasi hiyo kuwatakia waumini wote wa dini ya Kiislam heri ya kumalizia Ibada ya kufunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhani sambamba na kuingia kwenye sikukuu ya Idd.

Aidha Mashehe wa Jiji la Dar es Salaam waliohudhuria hafla hiyo jana walimpongeza Meya Mwita kwa kuandaa futari hiyo na kusema kuwa ni jambo la heri kwao na hivyo wataendelea kumuunga mkono katika shughuli zake za kuwaongoza wananchi kwa ajili ya kuwaletea maendeleo.

Hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa na Kadhi Mkuu wa Mkoa, Mashehe wa Jiji la Dar es Salaam, viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa, makundi mbalimbali ya kijamii, ilifanyika katika viwanja vya Karimjee jijini hapa.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa  futari hiyo jana Meya  Mwita alisema kuwa kupitia  mfungo wa Ramadhani  wakazi wa Jiji na watanzania wote kwa ujumla wanapaswa kuzidisha hali ya unyenyekevu, ucha Mungu ili kutenda mambo yaliyo mema na hivyo kusherehekea sikukuu ya Idd kwa hali ya utulivu.

Meya Mwita alifafanua kuwa kupitia hafla hiyo imekuwa ni fursa ya kipekee kujumuika pamoja na wananchi wa jijini hapa kuzungumza mambo mbalimbali ya maendeleo na kutumia nafasi hiyo kuwaalika kwenye ofisi za Jiji ili aweze kusikiliza kero zinazo wakabili na kuzipatia ufumbuzi wa haraka.

“Nimefarijika sana leo, kujumuika pamoja kwenye tukio hili muhimu ambalo hutokea kila mwaka, lengo la kuwa na hafla hili, ni kuungana na waumini wote wa dini ya  Kiislam wa jijjni hapa ambao wako katika mwezi mtukufu wa Ramadhani "

"Lakini pia hata wale ambao hawapo kwenye mfungo huu,  kupitia hadhara  hii tunaweza kukutana na wakazi wengi zaidi na kubadilishana mawazo”, alisema Meya Mwita. Jiji la Dar es Salaam lina wakazi wengi sana, ambapo huwezi kusema kwamba leo utakwenda kukaa na kila mmoja, lakini yapo matukio ambayo yanatukutanisha kama wanafamilia wa jiji la Dar es Salaam, na hii kwangu ndio faraja zaidi kwani tunakutana kwenye matukio ya kiimani, na siyo ya kisiasa.

Kwa upande wake  Shehe wa Wilaya ya Ilala Adam Mwinyipingu alimpongeza Meya Mwita kwa kuandaa hafla hiyo iliyomkutanisha na baadhi ya wananchi ambao walishiriki futari hiyo. Shehe Mwinyipingu alisema kuwa  jambo hilo ni la heri kwa waumini wote wa kiislam na wananchi wote waliohudhuria hafla hiyo ya futari.

Kwa upande wake  Mbunge wa Jimbo la  Temeke, Abdallah Mtolea pamoja na mambo mengine alimpongeza meya Mwita kwa kuandaa hafla hiyo, na kusema kuwa imesaidia kuwakutanisha na wananchi wao ambao si rahisi kukutana nao mara kwa mara  kutokana na shughuli zao.

“Kwa siku ya leo nimeifurahia nimeweza kujumuika na viongozi mbalimbali wa dini, vyama vya kisiasa, na wananchi wa Jiji hili ambao tunashindwa kukutana mara kwa mara kutokana na shughuli mbalimbali ambazo wametupatia wananchi ili kuwatumikia.



Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.