• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Meya wa Jiji la Dar es Salaam awashukia madereva wanaosafirisha wanafunzi

Posted on: June 22nd, 2017

MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amewataka madereva wanaowasafirisha wanafunzi wanaosoma shule nilizopo katikati ya Jiji kuwashusha na kuwachukua ndani ya kuta za shule badala ya kuwashusha na kuwachukua nje.

Meya Mwita aliyasema hayo jijini hapa leo wakati wa uzinduzi wa wiki ya Kimataifa ya usalama barabarani, ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa utaratibu wanaoutumia madereva hao ni hatari kwa wanafunzi  kwani inawalazimu  kuvuka barabara.

Alisisitiza kuwa iwapo watatumia utaratibu wa kushusha wanafunzi ndani ya kuta za shule itasaidia kupunguza hatari kwa wanafunzi ikiwemo kugongwa na gari, pikipiki, kupunguza msongamano wa magari barabarani.

“Jambo ambalo linakwenda kufanyika leo ni muhimu sana, limesaidia kuongeza usalama wa watoto wetu ambao wanasoma kwenye shule hizi zilizopo katikati ya Jiji, lakini pia linatoa nafasi kwa walimu kuwa na uhakika wa usalama wa  wanafunzi wao, najua wakati mwingine mmekuwa na wasiwasi kuhusu usalama wao.

"Nipende kutoa rai kwa madereva, zingatieni jambo hili, mabasi ya shule yawe yanachukua na kushusha wanafunzi ndani ya kuta za shule, utaratibu ambao mlikuwa mnautumia hivi sasa usitishwe mara moja.

Huko ni kuhatarisha maisha ya wanafunzi ambao baadae wangekuwa madokta, wabunge, marais tunawategemea. Watoto ndio Taifa la kesho, nawaomba sana walimu mlisimamie jambo hilo.

Aidha Meya Mwita aliwataka walimu na shule kwa ujumla kutumia kwa umakini vifaa vya usalama barabarani katika mitaala ya shule ili kuwafundishia wanafunzi masuala ya usalama barabarani kwani kutafanya watambue elimu hiyo na hivyo kuleta manufaa kwa Taifa.

Alisisitiza kuwa "elimu hii ikifundishwa vizuri itapunguza ajali za barabarani wakati wa kuvuka lakini pia hata pikipiki zitaendeshwa kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani bila kuathiri watumiaji wengine wa barabara”.

Hata hivyo Meya Mwita aliwapongeza Automobile Association Of Tanzania (AAT) na Federation International Automobile (FIA) kwa kuchukua jukumu la kupunguza ajali barabarani na kuokoa maisha ya wanafunzi.

Aidha AAT, FIA  kwa kushirikiana na kitengo cha Usalama barabarani elimu kwa umma, wamefundisha walimu 1,000 kutoka shule 51 za Jiji la Dar es Salaam kuhusu matumizi sahihi ya alama za barabarani na matumizi sahihi ya  barabara ambapo matarajio yake ni kuwafikia wanafunzi wengi zaidi.

Sambamba na hilo, AAT na FIA wameahidi kutoa elimu hiyo kwa kila Halmashuri za Jiji la Dar es Salaam ambapo jumla ya watu 10 watakuwa wakipatiwa mafunzo hayo.

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.