Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu leo tarehe 25 Machi, 2023 amekabidhi madawati 300 katika Shule ya Sekondari Ilala Kasuluiliyopo Kata ya Ilala ambapo Madawati 200 yametolewa na Mheshimiwa Zungu huku madawati 100 yakitoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inatekelezwa kwa kiasi kikubwa na kuhakikisha Sekta ya elimu inakua katika ufanisi na wanafunzi wote wanasoma katika mazingira bora na tulivu.
Akiongea katika hafla hiyo Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu ametoa shukurani zake za pekee kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na watendaji wake wote kwa kutatua kero ya madawati katika Shule ya Sekondari Ilala Kasulu huku akiwaahidi kuendelea kushirikiana nao katika kujenga na kuimarisha sekta ya elimu nchini, “Katika kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi tumeweza kutoa madawati 300 katika Shule yetu ya Sekondari Ilala Kasulu ambapo Juhudi zote hizi ni kutokana na jitihada za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kipaumbele katika Sekta ya elimu kwani kutokana na mchango wake katika kuipa kipambele elimu kwa kujenga Madarasa Katika Shule zetu hivyo na sisi hatunabudi kuleta madawati ili wanafunzi wetu waweze kusoma katika mazingira mazuri na salama.”
Aidha kwa upande wake Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi.Tabu Shaibu ameeleza kuwa “Katika utekelezaji wa Ilani ya Chama cha mapinduzi tumeweza kutekeleza na kukuza sekta ya elimu kukua katika ufanisi unaotarajiwa hivyo ni wahakikishie changamoto hizi zitaisha kabisa kwani tutashirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha tunamaliza changamoto zote zinazokabili sekta ya elimu katika Halmashauri yetu.”
Nae Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Ilala Kasulu Mwl. Hamis Ernesti Masatu amesema “Tunamshukuru sana Mbunge wetu pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kutupatia madawati 300 ambapo kwa kiwango chake tumepunguza idadi ya uhitaji wa madawati katika shule hii ya Sekondari Ilala Kasulu kwani tumepata nyongeza ya madawati takribani 86 hivyo wanafunzi wetu wataweza kusoma katika mazingira tulivu na idadi ya ufaulu itazidi kuongezeka. Pia tunaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani ya miaka hii miwili ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu tuliweza kupata fedha za madarasa ya Uviko ila kutokana na ufinyu wa eneo fedha hizo zikahamishiwa sehemu nyingine”.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.