Na: Doina Mwambagi
Kiasi cha Shilingi Milioni 750 kimetengwa kutoka fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kutekeleza mradi wa barabara ya mtaa wa Halisi Kata ya Majohe kwa kiwango cha zege.
Hayo yamebainishwa leo Januari 06, 2025 na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mheshimiwa Omary Kumbilamoto wakati wa ziara ya kukagua eneo hilo la ujenzi.
Akiongea wakati wa ziara hiyo Mhe. Kumbilamoto amemshukuru Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fedha anazotoa kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo huku akitoa wito kwa Wakandarasi kutekeleza miradi kwa muda uliopangwa ili waweze kutimiza adhma ya Serikali ya kuhakikisha huduma bora zinawafikia wananchi kwa wakati.
"Baada ya kuona eneo hili la Halisi barabarara yake haipitiki wakati wa mvua tuliamua kuanza utekekezeji wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha zege kwani asili ya eneo hili barabara ya lami haitadumu hivyo tumetoa milioni 750 kwa ajili ya utekelezaji wa barabara utakaoambatana na ujenzi wa mifereji mikubwa ya maji pamoja na taa 20 za barabarani" amesisitiza Mhe. Kumbilamoto.
Sambamba na hilo, Mhe. Kumbilamoto amewahakikishia wakandarasi wote wanaotekeleza miradi ya Jiji kuwa Fedha zao zitaingizwa kwa wakati ili miradi iliyokwama ikamilike kwa muda ukiopangwa.
Kwa upande wake Meneja wa TARURA Injinia Grayson Nzunda ameeleza kuwa Mradi huo uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 750 utatekelezwa mita 400 kwa kiwango cha zege na unatarajiwa kukamilika Julai 2025.
Naye Mkandarasi kutoka Osaka Constarction Injinia Joshua Warema ameahidi kukamilisha kazi hiyo kwa wakati kabla Mvua za Masika hazijaanza ili wananchi waondokane na adha hiyo na uharibifu wa barabara.
Barabara hiyo imekuwa kero na changamoto ya kupitika hasa kipindi cha mvua hali inayosababisha kupanda kwa gharama za maisha kutokana na usafiri kuwa wa shida kwa kipindi hicho.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.