Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amewataka wajumbe wa Kamati ya Lishe na Maafisa Watendaji wa Kata wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kutilia mkazo suala lautoaji wa vyakula mashuleni kwa Wanafunzi kwa kuwashirikisha walimu katika kutoa elimu bora kuhusu umuhimu wa Wanafunzi kupata chakula mashuleni ili kusaidia utekelezaji wa Afya ya Lishe kwa Wanafunzi itakayowawezesha kupata Elimu bora ikiwa ni sehemu ya agizo la Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Angellah Kairuki kama alivyoagiza katika ziara yake aliyoifanya katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Hayo ameyasema leo Februari 24, 2023 wakati walipofanya kikao cha kujadili tathmini ya utekelezaji wa Mikataba ya lishe ngazi ya Wilaya katika Ukumbi wa Mikutano wa Arnautoglo, na kuwataka watendaji wa Kata kutambua kuwa suala la utoaji wa vyakula mashuleni ni lazima na ni haki ya kila mwanafunzi kulingana na sheria na mwongozo wa nchi.
Aidha, Mhe. Mpogolo amewashukuru wajumbe wa Kamati ya Lishe pamoja na Watendaji Kata kwa utendaji wao kazi na kutoa mwezi mmoja kwa kila shule kuanzisha vilabu vya Afya ya lishe bila kusahau ushirikishwaji wa makundi maalumu wakiwemo Bodaboda, Mama lishe na Wamachinga.
Nae, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Tabu Shaibu amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Ilala kwa maelekezo aliyoyatoa katika kikao hiko cha tathmini ya utekelezaji wa Mikataba ya lishe na kumhakikishia kuwa wanaenda kutekeleza yale yote aliyoyaagiza ikiwemo utoaji wa Elimu Bora ya Afya ya lishe ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.