Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Ng’wilabuzu Ludigija leo tarehe 25 Novemba, 2022 amepokea vifaa kutoka kampuni ya Bora Rx Medisina na kuvikabidhi katika Zahanati ya Gerezani iliyopo katika Halmshauri ya Jiji la Dar es Salaam. Katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya amesema.
“Tunawapongeza kampuni ya Bora Rx Medicina kwa mchango wao katika Zahanati ya Gerezani ikiwa ni kuonyesha juhudi na kuungana na Serikali katika kudumisha huduma za afya hii kutokana na Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kudumisha ushiriano na mashirika Binafsi na sasa tunaona matunda haya yanawafikia wananchi”
Kampuni ya Bora imetoa vifaa vya kisasa vya matibabu na kuweza kufanya ukarabati katika kituo hiko ikiwa ni sehemu moja wapo ya kuunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kudumisha huduma bora za afya kwa Jamii.
Akitumia nafasi ya kuongea na wananchi walioudhuria hapo Mkurugenzi wa Kampuni ya Bora Rx Medicina Bi. Margareth Maganga amesema “Sisi ni watoa huduma ya famasia ambapo kwa sehemu kubwa tunajari ubora wa utoaji huduma,tunajali ushirikiano wetu na serikali pia sambamba na hilo tunaelimisha jamii kupitia mitandao ya kijamii juu ya matumiziya dawa bora na sio bora dawa”
Ikiwa ni uboreshaji wa huduma hizo nae Mfamasia wa kampuni ya Bora Rx Medicina ndugu Morris Mwinuka amesema “Baadhi ya vifaa ambavyo tumevikabidhi leo ni pamoja na vitanda vitano vya kufanyia uchunguzi, kitanda kimoja cha wodini, samani, darubini, semi-auta biochamp, coaqulation machine na vinginevyo vyenye thamani ya Shilingi Milioni 46 pamoja na ukarabati uliofanyika.''
Kwa kuhitimisha Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Eng. Amani Mafuru alitumia jukwaa hilo na kusema anashukuru kwa Kampuni kuunga mkono kazi zinazofanywa na Serikali lakini pia anafungua milango kwa kampuni zingine kuweza kushirikiana katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.