Katika kuendelea kuunga Mkono Juhudi za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan za kukuza sekta ya Michezo Nchini pamoja na kukuza vipaji vya vijana na kuwapa fursa ya Ajira, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Omary Kumbilamoto leo Septemba 12, 2024 amekabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi Milion 5.5 kwa timu 20 zitakazoenda kushiriki Kumbilamoto Cup 2024.
Akikabidhi vifaa hivyo katika Mtaa wa Mtambani Jijini Dar es Salaam, Mhe. Kumbilamoto ameeleza kuwa lengo la kuanzisha Kumbilamoto Cup ni kukuza vipaji vya vijana wa Jiji hilo pamoja na kuwatengenezea njianya kupata jira na kutimiza ndoto zao.
“Baada ya kufanya utafiti tumegundua vijana wenginwa Jiji la Dar es Salaam wanapenda Mpira hivyo Ofisi ya Mstahiki kwa kushirikiana na Kumbilamoto Foundation tukaona tuanzishe Kumbilamoto Cup kwajili ya kukuza vipaji lakini pia kuunga Mkono Juhudi za Mhe. Rais Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kukuza sekta ya michezo hivyo nitoe wito kwa Wadau wengine wa michezo kudhamini timu ndogondogo zinazoanza kwani huku mitaani vipaji ndo vilipo.”
Sambamba na hilo, Mhe. Kumbilamoto amemshukuru Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kwa kuona kuna tija ya kuhakikisha vipaji vinaibuliwa katika Jiji na vijana wanapata ajira na kutimiza ndoto zao za kuwa wachezaji wakubwa huku akieleza kuwa Mashindano Kumbilamoto Cup 2024 yanatarajiwa kufunguliwa rasmi Septemba 15, 2024 Katika viwanja vya Usikate Tamaa Vingunguti na zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washindi wote.
Kwa upande mwingine Mhe. Omary Kumbilamoto amewataka wananchi wa Kata ya Vingunguti kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura katika Mitaa yao ili kuweza Kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024 Sambamba na Kauli mbiu isemayo “Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi”.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.